Taasisi Zatakiwa Kutumia Sehemu ya Faida Kusaidia Jamii

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Prof. Emanuel Mjema (katikati), Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Kisarawe, Dk. Martin Msokelo(kulia) na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dk. Mohamed Mzige kwa pamoja wakitandika sehemu ya msaada wa mashuka 176 yaliyotolewa na CBE kwenye wodi ya Wazazi ya hospitali hiyo.

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Prof. Emanuel Mjema (katikati), Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Kisarawe, Dk. Martin Msokelo (kulia) na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dk. Mohamed Mzige kwa pamoja wakitandika sehemu ya msaada wa mashuka 176 yaliyotolewa na CBE kwenye wodi ya Wazazi ya hospitali hiyo.

Aron Msigwa -MAELEZO, Kisarawe

WITO umetolewa kwa Taasisi, mashirika na kampuni zote nchini kujenga utamaduni wa kutumia sehemu ya faida wanayoipata katika kuisaidia jamii kupitia sekta ya afya ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Wito huo umetolewa leo mjini Kisarawe na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Prof. Emanueli Mjema wakati akikabidhi msaada wa shuka 176 zilizotolewa na chuo hicho kusaidia wodi ya Wazazi ya Hospitali ya wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani.

Alisema CBE mwaka huu imetimiza miaka 50 toka kuanzishwa kwake mwaka 1965, hivyo ukongwe na umri wake nchini Tanzania umekua ukiendana na mabadiliko ya kiuchumi yanayotokea ndani na nje ya nchi ili kukidhi mahitaji na matarajio ya watanzania.

“CBE tukiwa chuo kikongwe nchini tumefanya mengi yenye manufaa kwa uchumi wa nchi yetu na jamii ya watanzania,kwa kuwathamini wananchi tunaowahudumia tuna utaratibu wa kurudisha sehemu ya faida tunayoipata kwa jamii na mwaka huu tulitenga kiasi cha shilingi milioni 9 kusaidia wodi za wazazi katika hospitali zetu,” Amesisitiza.

Alieleza kuwa ndani ya miaka 50, CBE imewanufaisha wananchi na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa kupitia Fani za Biashara, Ugavi na manunuzi, Vipimo, TEHAMA, Utawala katika biashara pamoja na kutoa huduma mbalimbali kwa jamii.

Amesisitiza kuelekea miaka 50 ijayo chuo chake kimeelekeza nguvu katika kuwekeza kwenye ubora na ujuzi wa kumuwezesha muhitimu kuitumia elimu aliyoipata kuleta manufaa na mabadiliko katika jamii inayomzunguka.

“Sisi kama chuo cha Elimu ya Biashara tumeona uhitaji uliopo nchini wa kukosa wataalam wenye ujuzi wa Biashara ndio maana tumeanza kufuandisha wanafunzi wa Shahada ya Elimu katika Biashara ili tupate wahitimu bora watakaokidhi mahitaji ya soko,” Amesisitiza.

Kwa upande, Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Dk. Martin Msokela akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo, ameushukuru uongozi wa CBE kwa kuwakumbuka wagonjwa wa Hospitali ya wilaya ya Kisarawe.

Amesema msaada uliotolewa na chuo hicho umepunguza uhitaji wa mashuka waliokuwa nao kwani Hospitali hiyo inakabiliwa na tatizo la uhaba wa mashuka kwenye vitanda vya wagonjwa. Dk. Msokela amewaomba wadau wengine kujitokeza kwa wingi kuisaidia hositali hiyo kama walivyofanya CBE ili kuboresha afya za wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kutibiwa.

“Nawaomba wadau wengine wajitokeze kusaidia kama walivyofanya CBE, licha ya hili la mashuka ukiangalia Jiografia ya Kisarawe, Hospitali yetu imekua na tatizo la upatikanaji wa maji na uchakavu wa mitambo,” Amebainisha.

Aidha katika hatua nyingine Dk. Msekela ameeleza kuwa hali ya ugonjwa wa Kipindupindu wilayani humo inaendelea kudhibitiwa kupitia timu ya wataalam iliyoundwa kukabiliana na tatizo hilo na kuongeza kuwa hospitali hiyo imepokea mgonjwa mmoja mwenye tatizo hilo.