Uboreshaji wa Usalama Barabarani kwa Usafirishaji wa Masafa Marefu.

Fuso ikipita Njiani kwenye Maonyesho ya "NDIO Fuso ni Faida" jijini Dar, Maonyesho hayo yanatarijiwa kupita kwenye Mikoa kama Tanga – Moshi- Arusha- Mwanza –Shinyanga -Kahama- Dodoma – Iringa – Mbeya  na Songea ambapo shughuli mbali mbali za uchimbaji wa madini, kilimo, ujenzi na usafirishaji wa mizigo zinafanyika

Fuso ikipita Njiani kwenye Maonyesho ya “NDIO Fuso ni Faida” jijini Dar, Maonyesho hayo yanatarijiwa kupita kwenye Mikoa kama Tanga – Moshi- Arusha- Mwanza –Shinyanga -Kahama- Dodoma – Iringa – Mbeya  na Songea ambapo shughuli mbali mbali za uchimbaji wa
madini, kilimo, ujenzi na usafirishaji wa mizigo zinafanyika

 
 Wadau wa Usafirashaji wakiwa katika Maonyesho ya ‘Fuso ni faida’ jijini Dar

Na Mwandishi Wetu,

Mtandao
wa miundombinu ya barabara nchini Tanzania inayokadiriwa kuwa na
kilometa za mraba 91,049 ambayo ni mara 30 zaidi ya mtandao wa reli
ambayo inaambaa kwenye eneo lenye ukubwa wa takribani kilomita za mraba
3,682 ikidhihirisha kuwa barabara ndiyo njia kuu inayopendelewa kutumika
katika usafirishaji wa mizigo.
Usafirishaji
nchini Tanzania unajumuisha mitandao ya barabara, anga, reli na maji
ambapo katika njia zote hizi, barabara na reli zinaongoza zikifuatiwa na
maji na anga.  Hakika katika suala la umbali, mtandao wa barabara za
Tanzania unashika nafasi ya 51 duniani, kutokana na taarifa
zilizonukuliwa katika kitabu “ CIA world fact book”
Wakati
ajali za barabarani zikiendelea kugharimu maisha ya watu, ufanisi wa
njia hii ya usafirishaji kwa ujumla wake unahitaji kudumisha ubora wa
usafirishaji wa barabara nchini Tanzania kutokana na ufanisi wake,
kuokoa mda na kuaminika pamoja na kuchukuliwa kuwa kiunganishi kikubwa
cha barabara ndogo kwenye barabara kuu za nchi.
Diamond
Motors limited hivi karibuni wamekuwa katika safari ya kuzunguka
mtandao huu wa barabara wakihamasisha pamoja na mambo mengine usalama
barabarani katika kampeni yao ya “Ndio! Fuso ni Faida” Kampeni hiyo
iliyozinduliwa mwezi julai mwaka huu jijini Dar es salaam ilifika katika
mikoa ya Tanga-Moshi- Arusha – Mwanza – Shinyanga – Kahama – Dodoma –
Iringa – Mbeya – na Songea ambapo shughuli mbali mbali za uchimbaji wa
madini, kilimo, ujenzi na usafirishaji wa mizigo zinafanyika. Pamoja na
mambo mengine, kampeni hiyo ilidhamiria kujenga uelewa kwa wateja wake
juu ya jinsi ya kuboresha usafirishaji salama wa mizigo kwa kutumia
magari ya kisasa zaidi.
Akifafanua
kwa undani juu ya malori mapya yaliyohusika katika kampeni hiyo ya
“Ndio! Fuso ni Faida” msemaji rasmi wa kampuni ya Diamond Motors Limited
ambao ni wadau na wataalamu katika sekta ya usafirishaji wa masafa
marefu kwa kutumia malori yao ya Fuso alisema soko la Tanzania
linahakikishiwa malori ya aina ya Fuso FZ na FJ yaliyoboreshwa
kiteknolojia na kuwa na uwezo wa kuboresha usalama barabarani.  “Malori
haya yametengenezwa na kitako imara kilichotengenezwa kwaajili ya uzito
mkubwa na mazingira magumu ya kufanya kazi” alisema Meneje Mkuu (Masoko)
wa diamond Motors Ltd bwana Laurian Martin.  Aliongeza kusema kuwa
“tuna nia ya kuborsha sekta ya usafirishaji iliyo bora na salama kwa
kutumia malori yetu ya Fuso yaliyo boreshwa ki teknolojia”
Alisistiza
na kusema kuwa “aina mbali mbali mpya za malori yatolewayo na Diamond
Motors Ltd sio yanaaminiki katika utendaji tu, bali pia yana uwezo
mkubwa wa ubebaji ambayo ni sifa pekee isiyopatikana katika malori
mengine ambayo yanalazimika kutumia mafuta mengi ili kukidhi kigezo
hicho. Kizuri zaidi, malori haya gharama zake za matengezo ni ndogo
zaidi na hutembea umbali mrefu zaidi wa takribani kilomita 45,000 kabla
ya kuhitaji matengenezo ya kawaida kama kubadilisha vilainishi”.
Bwana
Laurian Martin aliendelea kusema kuwa “Sifa hizi ndizo zinafanya malori
ya Fuso FZ na FJ kuwa suluhisho kamili la usafirishaji na biashara
nchini Tanzania”. Katika kampeni hiyo mikoa ya kaskazini ikiwemo Tanga,
Kilimanjaro, na Arusha ilipata  fursa ya kuona faida zinazopatikana
katika malori haya mbalimbali ya Fuso maboyo ni malori ya ubebaji mkubwa
yanayopatikana katika kampuni ya Diamond Motors Ltd.  Miji ya mikoa hii
imendelea kukua katika shughuli za kiuchumi kama vile usafirishaji wa
mizigo, biashara, viwanda kama vile cementi, malighafi mbalimbali, maua,
matunda, mazao mbalimbali yatokanayo na miti yanayohitaji kusafirishwa
kwenda katika sehemu mbalimbali za nchi na nje ya nchi.  Wasafirishaji
kutoka mikoa hii wameaswa kutumia teknolojia hii ya malori ya Fuso FZ na
FJ ambayo inaweza kuwapatia Faida zaidi katika biashara zao.
Kampeni
hiyo pia  ilifika katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambayo
imeunganishwa katika ukanda wa kaskazini na barabara za nchi za jirani
kama Kenya na Uganda kupitia mipaka yake ya Namanga ikiwa na biashara
nyingi baina ya nchi hizo zinazopitia njia ya barabara.  Wakazi na
wafanyabiashara waliohudhulia kampeni hiyo walipata fursa ya kujionea
sifa zipatikanazo katika malori hayo ya Fuso Fz kutoka Diamond Motors
Limted ambayo yanauwezo wa kubeba mizigo mikubwa katika mazingira magumu
katika ukanda huo.  “Ni kwa teknolojia ya kisasa ya magari haya mabapo
wafanya biashara wanaweza kupata Faida ya biashaza zao kwa kutumia
malori haya inayotumia mafuta vizuri, ambapo gari hii ina kifaa maalumu
cha kuzuia mafuta yasitumike endapo gari hii inatembea katika mteremko
ili kukupa umbali mrefu zaidi kwa mafuta kidogo.
Mikoa
ya Mwanza na Shinyanga ambayo ni kitovu cha biashara, usafirishaji,
ushirikano wa kikanda na maendeleo ya kiuchumi katika kanda ya ziwa
ikiunganishwa na bandari kavu ya Isaka, ilifikiwa na maonyesho haya ya
Fuso Fz.  Mikoa hii pia inaunganisha nchi jirani za Uganda, Kenya,
Rwanda, Burundi and Demokrasia ya Kongo ambazo ni nchi zenye biashara
nyingi kubwa miongoni mwake na Tanzania.
Kwa
usafirishaji wa masafa marefu katika nchi hizi, Fuso Fz ina muundo
maridhawa kupasua upepo usiwe kizingiti ambayo haikupatii umbali mrefu
tu, bali pia inampunguzia dereva uchuvu kwa kuwa na kibini
iliyoninginizwa vizuri kupumguza sana mtikisiko wa barabarani hasa
kwenye matuta au barabara mbovu na kupunguza kelele za kutoka kwenye
injini.  Sifa hii ni muhimu sana kumpunguzia dereva uchovu na hivyo
kuweza kutosababisha ajali zitokanazo na uchvu wa dereva na kusinzia
wakati akiendesha. 

Mikoa
ya nyanda za juu kusini pia ilikuwa katika mpango wa kupata faida
zitokanazo na matumizi ya malori mapya Fuso Fz yenye teknolojia mpya
kutoka Diamond Motors ltd baada ya kufikiwa na kampeni hiyo ya “Ndio!
Fuso ni Faida” Kampeni hiyo ilipokelewa vizuri na wakazi wa mikoa ya
Dodoma, Iringa, Mbeya na Songea ambapo pia kuna shughuli za kiuchumi
kama uchimbaji wa madini, kilimo cha chai, misitu na kilimo cha
kibiashara.  Wafanyabiashara walionyeshwa haja ya wao kubadilisha njia
za usafirishaji kwa kutumia Fuso Fz na Fuso FJ na hivyo kupunguza
gharama za uendeshaji na kupata Faida zaidi katika biashara za kiuchumi
nchini na ukanda wa Africa Mashariki na kati.