Shirika la Maendeleo Tarime SHIMATA chini ya ufadhiri wa Taasisi ya TWAWEZA kupitia mradi wake wa UWEZO ambao umelenga kufanya kazi ya kutathimini hali ya kielimu katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda linatarajia kufanya tathimini kwa watoto (Wanafunzi na wasio wanafunzi) walio na umri kati ya miaka saba hadi 16 katika Wilaya ya Tarime Mkoani Mara kwa lengo la kubaini hali ya kielimu na changamoto zake ilivyo wilayani humo.
Ili kufanikisha zoezi hilo, SHIMATA imetoa semina kwa wahojaji watakaofanya tathimini hiyo ambayo pia itawafikia wenyeviti wa Mitaa na Vijiji pamoja na Wanakaya pamoja na kupima kiwango cha madini joto katika kaya hizo.
Akifunga semina hiyo iliyoanza juzi Septemba 22,2015 na kutamatika jana Septemba 23,2015 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Tarime John Marwa ambae alimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo aliwataka washiriki wa semina hiyo (wahojaji) kuhakikisha wanafanya tathimini hiyo kwa ukweli na uwazi ili kupata majibu sahihi ya kiwango cha elimu katika Wilaya hiyo.
Mwenyekiti wa SHIMATA Joseph Magabe akizungumza katika semina hiyo
Baada ya semina, mgeni rasmi alikabidhi vyeti vya ushiriki kwa wanasemina

Mratibu wa Twaweza Wilayani Tarime akipokea Cheti cha utambuzi kutoka TWAWEZA
Mwenyekiti wa SHIMATA akipokea cheti cha utambuzi kutoka TWAWEZA
Picha ya pamoja kati ya washiriki wa semina na mgeni rasmi

Viongozi na Wajumbe wa SHIMATA. Chanzo: Binagi Media Group