Msafara wa Sugu Washambuliwa kwa Mawe

 

Gari la Mgombea Ubunge jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi Sugu likiwa kituo cha Polisi kati jijini Mbeya mara baada ya kushambuliwa kwa mawe na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa CCM

 

(JAMIIMOJABLOG MBEYA )

 

Na Emanuel
Kahema ,Mbeya

 

 

MGOMBEA
ubunge  kupitia chadema jimbo la Mbeya
mjini, Joseph Mbilinyi leo  amejikuta
katika wakati mgumu baada ya msafara wake kushambuliwa na mawe na wafuasi wanaosadikiwa
kuwa ni wa chama   cha mapinduzi CCM na kwamba katika tukio hilo
watu wawili wamejeruhiwa akiwemo dereva aliyekuwa akimuendesha mgombea huyo  .

 

 

Tukio hilo
la kushambuliwa kwa msafara huo, limetokea majira ya saa 11 za jioni katika
eneo  la barabarani lililopo katika Kata
ya Ghana mtaa wa Mbata jijini hapa  ambapo inasemekana mgombea huyo alikuwa  katika harakati za kampeni kuomba kura kwa
wananchi wa Iziwa  ambapo mgombea huyo
alikuwa ndani ya gari yake yenye namba za usajili T161 CPP Toyota  Land Cruser VX .

 

 

Awali, wafuasi
wa chama cha mapinduzi CCM, walikuwa katika mkutano wa hadhara wa kumnadi
mgombea wao ngazi ya Udiwani katika kata ya Ghana iliyopo ndani ya Jiji la
Mbeya, hivyo wakiwa kwenye harakati hizo inasemekana walishangaa kuona msafara
wa sugu ukipita katikati ya mkutano huo hivyo kushindwa kuvumilia na kuanza
kurusha mawe huku wengine wakishikana mithili ya kutaka kupigana.

 

 

 

 

Katika
vurugu hizo gari aliyokuwa amepanda mgombea huyo  lilipasuliwa kioo cha mbele na gari ya chama
cha mapinduzi CCM wilaya ya Mbeya, ikipasuliwa kioo cha mbele .

 

 

Aidha Vurugu
hizo zimesababisha   majeruhi wawili ambao wamelazwa katika
hospitali ya Rufaa ya Mbeya akiwemo dereva wa mbunge huyo na mfuasi mmoja wa
chadema.

 

 

Kutokana na
hali hiyo  mgombea huyo wa ubunge mbeya
mjini kwa tiketi ya Chadema alilazimika kuikatisha zoezi lake la kuongea na
wakazi wa Kata ya Iziwa iliyopo Jijini Mbeya kwa muda, kutokana na kulazimika
kuripoti katika kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa maelezo.

 

 

Mgombea huyo
ilimlazimu kufika kituoni na kuchukuliwa maelezo na baada ya hapo aliruhusiwa
kuendelea na shughuli zake za kisiasa lakini gari yake yenye namba za usajili
T161 CPP aliyokuwa akiitumia katika kampeni zake ikibaki polisi.

 

 

 

 

Hata hivyo,
mgombea huyo alipomaliza kutoa maelezo
katika kituo cha polisi cha kati cha Wilaya ya Mbeya, aligoma kuzungumza
na vyombo vya habari ambavyo vilikuwa kwenye eneo la tukio na kuwataka wafike
katika mkutano kwani ndipo atakapotolea ufafanuzi wa suala hilo hilo.

 

Mwisho.