Dk. John Magufuli; Sipo Tayari Kutoa Matumaini Hewa

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa kiutendaji zaidi ili kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa jumla.

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa kiutendaji zaidi ili kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa jumla.

 
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa kiutendaji zaidi ili kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa jumla.
 
  Wananchi wa mji wa Ifakara waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM ndani ya uwanja wa saba saba wilayani Kilombero, wakimshangilia kwa shangwe Mgombea Urais wa CCM Dk. Magufuli alipowahutubia kwenye mkutano huo.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha mgombea ubunge jimbo la ilombero Abubakar Assenga almaarufu kama mtoto wa fundi Cherehani kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika Ifakara wilayani Kilombero.
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli amesema iwapo atachaguliwa katika uchaguzi mkuu mwaka huu na kufanikiwa kuunda Serikali yake atahakikisha baadhi ya mambo ya msingi atayaamua kwa kupata ushauri wa marais waliomtangulia, amesema kuwa katika kipindi hiki cha kuomba ridhaa ya wananchi ili awe Rais hatakuwa tayari kutoa matumani hewa ambayo anajua wazi hayatekelezeki kwani ni dhambi na kufafafanua kila anachoahidi anauhakika anao uwezo wa kutekeleza.
 
Akizungumza kwenye mikutano yake mbalimbali ya kuomba ridhaa ya kuwania urais, Dk. Magufuli aliwambia wananchi wa Ulanga kuwa anatambua dhamana anayoomba kwa wananchi lakini ana uhakika malengo yake ya kuwatumikia Watanzania na kuleta maendeleo yatafanikiwa kwani iwapo atahitaji ushaauri ataupata kwa viongozi
waliomtangulia kuongoza nchi.
 
Alisema sifa kubwa ya Tanzania ni kwamba kuna viongozi wastaafu wengi wakimo marais
ambao wametanguli kuongoza nchi kuanzia awamu ya pili, ya tatu na awamu ya nne.
“Iwapo nahitaji ushauri, wapo viongozi wengi wa kunisaidia kuniongoza. Yupo mzee Ali
Hassan Mwinyi(Rais awamu ya pili), Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Rais Jakaya
Kikwete, Rais mstaafu Salimn Amour na Rais mstaafu Aman Abeid Karume.
 
“Huu ndio utaratibu wan chi yetu kwamba wapo viongozi wa kutosha wa kunipa ushauri
katika kutekeleza majukumu yangu ya kuwatumikia Watanzania. Najua msimamo wangu
na Serikali nitakayoiunda ni kufanya kazi tu. Narudia tena kwangu mimi ni kazi
tu lakini bado ninao wazee wa kunishauri ili nifikie malengo yangu,”alisema.
 Alisema kiongozi mzuri ni Yule ambaye anaweka malengo ya kuwatumikia wananchi kwa
misingi ya uzalendo na uadilifu na anapoona kuna mambo yanahitaji ushauri kabla
ya kufikia uamuzi wapo viongozi wa kumshauri na kumpa mbinu za kufanya.
 
Dk. Magufuli ameanza awamu ya pili ya kampeni baada ya kumaliza mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Mkoa mmoja wa Kusini wa Mtwara ambapo jana ameanza ziara Mkoa wa Morogoro.
 
 Msafara wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli  ukikatiza kwenye dara la muda la Mto Kilombero, ambalo hutumika kupitishia vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenze wa daraja kubwa linalojengwa katika mto huo wa kilombero.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli  akikagua daraja la Mto kilombero ambalo ujenzi wake unaendelea mpaka sasa. 
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli  akipata maelezo mafupi kuhusia na maendeleo ya ujenzi wa dara hilo ambalo litakuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi wa Kilombero, litapunguza kero kubwa ya usafiri miongoni mwao kwa kiasi kikibwa.
 Baadhi ya Viongozi wa Dini wakimwombea sala  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli  mara baada ya kumaliza kuhutubia kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Mahenge jioni.
 
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Ifakara wilayani Kilombero kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa wakati wake utakuwa wa kiutendaji zaidi ili kufanikisha maendeleo ya haraka kwa nchi na wananchi kwa jumla.
 
 Wanafuatilia kwa makini yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye mkutano huo wa kampeni za CCM mjini Ifakara
 
 Mkutano wa kampeni za CCM ulipokuwa ukiendelea katika uwanja wa saba saba mjini Ifakara wilayani Kilombero.
 Mfuasi wa CCM na bango lake
  Wananchi wa mji wa Ifakara waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM ndani ya uwanja wa saba saba wilayani Kilombero, wakimsikiliza kwa makini mgombea Urais wa CCM Dk. Magufuli alipowahutubia kwenye mkutano huo.
  mgombea ubunge jimbo la ilombero Abubakar Assenga almaarufu kama mtoto wa fundi Cherehani akizungumza jambo kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika Ifakara wilayani Kilombero.
 Wananchi wa mji wa Ifakara walaiojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM ndani ya uwanja wa saba saba wilayani Kilombero, wakimsikiliza kwa makini mgombea Urais wa CCM Dk. Magufuli alipowahutubia kwenye mkutano huo. 
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM Mgombea Udiwani wa CCM wilaya ya Ulanga kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msinfi Mahenge.
 Wananchi wakifuatilia hotuba ya Magufuli alipokuwa akipita kuwasalimia wananchi wa kijiji cha Lupiro-Ifakara wilayani Kilombero
nanchi wa kijiji cha Lupiro-Ifakara wilayani Kilombero wakiwa wamefunga bara bara wakimsimamisha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli  awasalimie alipokuwa akitokea Malinyi
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi, Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa mji wa Ifakara waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Saba saba.