Serikali Kuzingatia Ripoti ya ESRF ya Maendeleo ya Binadamu

Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia na meza kuu katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa waliodhuria warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia na meza kuu katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa waliodhuria warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

IMG_4862

Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia (kushoto) akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dk. Tausi Kida (katikati) pamoja Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kuelekea sehemu maalum ya mapumziko kabla ya kuingia katika ukumbi wa mikutano.

IMG_4966

Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh. Hawa Ghasia akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya uwasilishaji wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya iliyofanyika jijini Arusha katika hoteli ya Ngurdoto.

IMG_4954

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dk. Tausi Kida (katikati) pamoja Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakifuatilia kwa ukaribu hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani).

IMG_4927

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

IMG_4990

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 na Wakuu wa mikoa, wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa mikoa iliyofanyika katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

IMG_5217

Naibu Mkurugenzi Mkazi, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Amon Manyama akiwasilisha mada ya Mageuzi ya kiuchumi yanayoendelea: kuangalia zaidi ukaji wa uchumi wakati wa warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa kwa Wakuu wa mikoa, wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa mikoa katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

IMG_5012

Mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone (kushoto) wakifuatilia kwa umakini na viongozi wenzake wakati mada mbalimbali zizokuwa zikiwasilishwa kwenye warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa jijini Arusha.

 

IMG_5019

Wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa waliohudhuria warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

 

IMG_5110

Mgeni rasmi na meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF).

Na Mwandishi wetu, Arusha

SERIKALI imesema itazingatia ushauri uliotolewa katika Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania ya Mwaka 2014 iliyowasilishwa kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya katika warsha yao iliyofanyika Ngurdoto, Arusha.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh. Hawa Ghasia wakati akifungua warsha yenye lengo la kujadili na kuielewa.

Ripoti hiyo ambayo imejadiliwa kama “Mageuzi ya Kiuchumi kwa Maendeleo ya Binadamu” ilizinduliwa rasmi mwezi machi mwaka huu wa 2015 inawasilishwa kutokana na haja ya viongozi hao kutambua yaliyomo na namna ya kusonga mbele katika mipango ya baadae.

Ripoti hiyo ambayo ni matokeo ya utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imelenga kusaidia kufahamu yaliyomo katika ripoti hiyo ili kuwawezesha viongozi hao kupata uelewa mpana juu ya dhana hii ya masuala ya Maendeleo ya Binadamu.

Warsha hiyo imewezesha na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Ghasia alisema utafiti huo umelenga kuzijengea uwezo mamlaka za mikoa na serikali za mitaa ili kuziwezesha kutoa huduma bora kwa wananchi.

Ripoti hiyo ambayo imezungumzia masuala ya mageuzi ya kiuchumi kwa Maendeleo ya Binadamu imetafakari kwa undani namna ya kufanya mageuzi ya kiuchumi katika taifa ili kuleta maendeleo ya Binadamu.

Akizungumzia maendeleo alisema mwanzoni mwa karne ya 21, mataifa mengi ya kiafrika yalitengeneza Dira za Maendeleo kuwa mwongozo wa ujenzi wa uchumi na maendeleo.

“Kwa upande wa taifa letu, Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025 inalenga katika kulifanya taifa letu kuwa nchi ya uchumi wa kati wenye kutegemea zaidi sekta ya viwanda na huduma.

“ Kwa maneno mengine, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 inalenga siyo tu katika ukuzaji wa uchumi bali kubadilisha muundo wa uchumi; kwa miaka mingi uchumi wa Taifa letu umekuwa unategemea zaidi kilimo ambacho kina tija ndogo.” alisema Ghasia.

Alisema kwamba Sera za Maendeleo ya taifa letu tangu uhuru zimekuwa zikiweka kipaumbele katika dhana ya Maendeleo ya Binadamu.

“Kwa mfano, Azimio la Arusha la mwaka 1967, ambalo liliamua taifa lifuate mfumo wa ujamaa na kujitegemea lilielekeza kwamba sera, mipango na mikakati yote lazima zizingatie uboreshwaji wa maisha ya watu kwani lengo la maendeleo ni watu.” Alisema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akizungumzia warsha hiyo alisema kwamba utafiti huyo uliofanywa na taasisi yake uliwezekana kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Idara ya uchumi), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali ya Zanzibar.

Alisema Toleo hilo la Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania ya 2014 ni toleo la kwanza nchini.

Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo hapa nchini na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, alizungumzia umuhimu wa mabadiliko ya kiuchumi ili taifa liwe la kipato cha kati.

Alisema ipo haja kwa taifa hili kuhakikisha kwamba linatumia vyanzo vyake vya kifedha kubadilika kutokana na hali halisi ilivyo kwa sasa.

Aidha alisema ipo haja ya kuzingatia mipango madhubuti ya kuondoa umaskini na kulinda mazingira, mambo ambayo yapo katika mpango mkakati wa Umoja wa Mataifa wa UNDAP wa maendeleo kuanzia mwaka kesho hadi 2021.