Ofisa ugavi mahakamani kwa kugushi vyeti vya taaluma

Na Janeth Mushi, Arusha

ALIYEKUWA Ofisa Ugavi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Elizabeth Kisanga jana amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kwa kosa la kugushi vyeti vya sekondari na vya taaluma ya ugavi, kinyume cha taratibu na sheria.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya hiyo, Devotha Msofe, Wakili wa Serikali, Sabina Silayo, aliieleza Mahakama kuwa mshitakiwa anakabiliwa na makosa matano.

Silayo alitaja miongoni mwa makosa hayo kuwa ni kughushi vyeti vya
Sekondari, vyeti vya taaluma ya Ugavi na kumdangaya mwajiri na kupata ajira hiyo kwa zaidi ya miaka 10. Aidha mshitakiwa baada ya kusomewa hati ya mashitaka hayo, alikana na kupewa dhamana, hadi kesi hiyo itakapoanza kusikiliwa Septemba 13
mwaka huu.

Hakimu Devotha, alihairisha kesi hiyo na kutaka upande wa mashitaka
kupeleka mashahidi pindi shauri hilo litakapoanza kusikilizwa.