Soma Mapendekezo ya Ilani ya Asasi za Kiraia kwa Wanasiasa


SIFA ZA KIONGOZI ANAYEFAA

CHAGUZI ni sehemu kuu ya michakato ya kidemokrasia duniani kote. Sisi asasi za
kiraia tukiwa watetezi na wasimamizi wa demokrasia, utawala bora na haki za
binadamu, hatumuungi mkono mgombea yeyote wala chama chochote cha kisiasa
kinachotafuta kuingia madarakani wala hatulengi kuchukua dola. Kwa ujumla wake,
uchaguzi huundwa na wadau wengi lakini makundi makuu mawili ni wapiga kura na
wapigiwa kura. Ili wapiga kura waweze kuchagua kiongozi atakayeweza kusimamia
maendeleo ya nchi na kuhakikisha amani ya nchi inazidi kudumu haina budi kuwa na vigezo
vya kiongozi bora. Vigezo hivyo ndiyo dira inayoongoza asasi zote na wananchi kwa ujumla
kuwapigia kura wanaotafuta ridhaa ya kuingia madarakani.
III.ii. Kiongozi Anayefaa ni Yupi?
Hivyo basi, kwa kutambua jambo umuhimu wa kuw ana kiongoi anayefaa, Asasi za Kiraia
(AZAKI) kwa umoja wetu tunakumbusha kuwa kiongozi anayefaa kuiongoza Tanzania
tuitakayo ni:
 Mtetezi na mlinzi wa katiba na haki za binadamu.Hii ni sifa kuu kwa kiongozi yeyote
yule kuanzia ngazi za chini za serikali mpaka ngazi za juu. Kiongozi bora ni yule
anayeweza kusimamia, kutetea na kulinda haki za binadamu.
 Awe na utashi na busara za kiuongozi na asiyekubali kupitisha na kusimamia sheria
mbovu zenye kukandamiza haki za binadamu.
 Ni muwazi katika utendaji kazi wa serikali na anayethamini ushirikishwaji wa
wananchi katika mipango ya umma kwa maendeleo ya taifa. Kiongozi anapaswa
kuwa muumini wa maendeleo shirikishi yatakayoweza kuinua uchumi na kutengeneza
mazingira rafiki ya ajira.
 Ni muwajibikaji na aliyetayari kufanya maamuzi yenye tija kwa taifa pamoja na
kuwawajibisha viongozi wengine wa umma wanaposhindwa kutekeleza majukumu
yao bila kuvunja sheria za nchi.
 Ni mwadilifu, asiyetoa wala kupokea rushwa, mzalendo kwa nchi yake na aliye
tayari kuondoa mifumo ya rushwa na ubadhirifu nchini.
 Ni mahiri katika kusimamia na kulinda rasilimali za nchi yetu ikiwemo kupinga
mikataba ambayo haina tija kwa nchi yetu.
 Anayeamini kwa dhati katika misingi ya usawa wa kijinsia kwa mapana yake.
U
9
VIPAUMBELE VIKUU VYA AZAKI
(i) Katiba Mpya
Tukukumbuke kuwa mchakato wa kuandika katiba mpya ulikwisha anza na umetumia pesa
nyingi za Watanzania. Ni wazi kuwa hadi tunapokwenda kupiga kura Octoba 25 mwaka huu
mchakato wa Katiba mpya hautakuwa umekamilika, kwa mantiki hiyo sisi wana AZAKI
tunawataka wagombea wanaotafuta ridhaa ya uongozi watumie muda wa kampeni
kuwahakishia watanzania kuwa wataendeleza mchakato wa upatikanaji wa katiba ya
wananchi ndani ya muda wa miaka miwili. Pia wahakikishie wananchi kuwa watarurudisha
misingi ya upatikanaji wa Katiba kwa kuweka mazingira yatakayoheshimu maoni ya
wananchi na kujali ushiriki wa wananchi wote katika kutunga Katiba ya Taifa lao.
(ii) Sera ya Uchumi wa Kitaifa
Tunataka kiongozi ambaye anatambua kwamba pamoja na kuwa kwenye uhuru zaidi ya
miaka 50 watanzania wengi bado ni masikini licha ya kuwa Taifa hili lina utajiri mkubwa.
Tunamhitaji kiongozi atakayeweza kuja na sera ya Uchumi wa Taifa yenye malengo ya
kulikwamua Taifa kiuchumi kwa kujenga mazigira sawa ya kiuchumi kwa watanzania wote
bila kuweka matabaka ya walinacho na wasionacho. Tunahitaji kuona sera ya Taifa ya
uchumi itakayosaidia kuliinua Taifa la kutoka kwenye Taifa linalotegemea misaada na kuwa
taifa linajitegemea kiuchumi kwa kuongeza uzalishaji wa ndani, kukuza viwanda vya ndani
na kupunguza matumizi yasiyo lazima ya serikali.
(iii) Usimamizi wa Rasilimali za Umma
Tanzania ni mojawapo ya nchi zilizobarikiwa kuwa na rasilimali ambazo ni ardhi, madini,
gesi asilia, mafuta, bahari, maziwa, mito, wanyama pori na misitu asilia. Katika miaka ya hivi
karibuni ulinzi thabiti wa rasilimali za nchi hususan kwa mamlaka husika umekosekana
nchini hali inayosababisha upotevu na ubadhirifu wa rasilmali za nchi kwa mfano, uvunaji
haramu wa rasilimali misitu na bahari , umilikishwaji wa ardhi ya wazawa kinyume na sheria
pamoja na ujangili wa wanyamapori. Pia tumeona viongozi wakiingia mikataba ya uwekezaji
uvunaji na wa rasilimali isiyo na tija kwa taifa. Tunawataka viongozi wote wenye kuwania
nafasi za uongozi kutamka bila kificho namna watakavyosimamia na kulinda rasilimali za
nchi ili zitumike kwa manufaa ya Taifa na watu wake.
(iv) Haki za Binadamu, Utawala wa Sheria na Mgawanyo wa Madaraka
Tanzania kwa muda mrefu sasa imekuwa na changamoto kubwa kuhusu utawala wenye
kufuata misingi ya sheria, haki za binadamu na mgawanyo wa madaraka. Tunahitaji kuona
Tanzaia yenye viongozi watakaoweza kusimamia utawala wa sheria, kulinda haki za
binadamu na missing ya mgawanyo wa madaraka. Kama njia ya kutekeleza haki za
binadamu, pia tunawataka viongozi watakaochaguliwa waweke nguvu zaidi kwenye
kuboresha huduma za msingi za kijamii kama vile elimu na afya.
10
SURA YA KWANZA
DHANA NA UMUHIMU WA UCHAGUZI
1.0 Dhana ya Uchaguzi
aki za binadamu hususan haki za kisiasa na kiraia zinafafanua uchaguzi wa
kidemokrasia kuwa ni mchakato mzima wa kupata viongozi wa ngazi mbalimbali
za serikali kwa kuchaguliwa na wananchi. Uchaguzi ni mchakato wa kuwapata
viongozi kwa njia ya kidemokrasia kupitia sanduku la kura.
Hapa Tanzania kuna aina zifuatazo za uchaguzi kwa mujibu wa Katiba na sheria;
o Uchaguzi mkuu ambao huwawezesha wananchi kuwachagua viongozi
wakuu wa taifa Rais, wabunge na madiwani kwa Tanzania bara na kwa
upande wa Zanzibar huwachagua Rais wa Zanzibar na Wajumbe wa Baraza la
wawakilishi na Madiwani.
Uchaguzi wa serikali za mitaa ambao hujumuisha uchaguzi wa wenyeviti wa vijiji,
mitaa, vitongoji na wajumbe wa serikali ya kijiji na mtaaKwa kifupi, mchakato wa
uchaguzi nchini Tanzania unajumuisha;
o Haki ya kuchagua na kupiga kura ambayo imeainishwa katika ibara ya 5(1) ya Katiba
ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya Mwaka 1977 (toleo la 2005) na Katiba ya
Zanzibar ya 1984 (toleo la 2010)
o Haki ya kuchaguliwa na kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi kama
ilivyoainishwa katika ibara ya 21(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1.1 Umuhimu wa Uchaguzi
Uchaguzi ni mchakato muhimu sana katika taifa letu kwani ndio hatua pekee ya
kidemokrasia inayowezesha kupatikana kwa viongozi wenye jukumu la kuongoza na kuleta
maendeleo katika nchi husika kwa kufuata na kutekeleza sera, sheria, kanuni na malengo ya
nchi. Kwa ujumla umuhimu wa uchaguzi ni;
o Kutekeleza dhana ya mamlaka na madaraka yote ya serikali yanatokana na wananchi
kama ilivyo ainishwa katika ibara ya 8(1)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Kupata viongozi wa nchi kwa ngazi mbalimbali kwa njia ya kidemokrasia
o Kuheshimu utawala wa katiba na sheria kwa kutekeleza haki zilizoainishwa katika
sheria na Katiba ya nchi.
o Kuwapa nafasi wananchi kushiriki katka shughuli za utawala wa nchi na utekelezaji
wa mambo muhimu ya ujenzi na maendeleo ya nchi.
H
11
o Kuwapatia wananchi na viongozi fursa ya kujadiliana kuhusu changamoto za maisha
ya watu na namna bora ya kuzitatua.
o Ni fursa kwa wagombea kuwasikiliza wananchi na kunadi ilani ya vyama vyao, ikiwa
ni pamoja na wananchi kuwawajibisha viongozi wazembe na walioshindwa kutimiza
malengo na matarajio ya wananchi.
1.2 Umuhimu wa Kupiga Kura
o Kwa kupiga kura, mwananchi anayo nafasi ya kutimiza haki yake ya kikatiba ya
kushiriki katika ujenzi wa maendeleo ya nchi na upatikanaji wa huduma muhimu
za kijamii na kiuchumi kwa faida yake na vizazi vijavyo.
o Kura inatoa nafasi ya kidemokrasia kwake kama mwananchi kukasimisha
madaraka na mamlaka ya kikatiba aliyonayo kwa serikali kupitia wawakilishi.
o Kura inatoa nafasi kwa wananchi kukasimisha usimamizi wa rasimali kwa
viongozi.
o Kura inatoa fursa kwa wananchi kunufaika na matumizi ya kodi wanazolipa
o Kura ikitumika vizuri inaweza kutatua matatizo ndani ya jamii.
1.3 Vigezo vya Uchaguzi Huru na wa Haki
Uchaguzi unapaswa kuwa huru na wa haki ili kuzingatia demokrasia na utawala wa sheria.
Vifuatavyo ni vigezo vya uchaguzi huru na wa haki vinavyopaswa kuzingatiwa katika
mchakato wa uchaguzi nchini;
o Watu wote wenye sifa na vigezo vya kushiriki katika uchaguzi kwa mujibu wa
katiba na sheria za nchi wanashiriki kikamilifu (Universal suffrage).
o Kura inakuwa ni siri ya mpiga kura.(secret ballot )
o Uchaguzi unakuwa wa moja kwa moja yaani kura moja mtu mmoja.
o Usawa unakuwepo na kulindwa baina ya wapiga kura wote na vyama vya siasa
vinavyoshiriki katika uchaguzi.
o Uwepo wa sheria za uchaguzi zilizo huru na zinazofuata misingi ya demokrasia
o Uwepo wa ushindani wa ukweli wa kisiasa baina ya vyama vya siasa hapa nchini
1.4 Hatua Muhimu za Mchakato wa Uchaguzi
Ili uchaguzi uweze kuwa huru na wa haki lazima mchakato mzima uhusishe hatua muhimu
zifuatazo;
(A) Maandalizi ya uchaguzi
 Utungwaji shirikishi wa sheria za uchaguzi na utekelezaji
12
 Uhamasishaji/elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki katika
uchaguzi.
 Uandikishaji wa wapiga kura unaozingatia vigezo vya kikatiba na sheria za
nchi.
 Kampeni za uchaguzi ili kuwapa wanananchi fursa ya kuchagua kiongozi
wanae mtaka.
(B) Wakati wa Kupiga kura
 Upigaji kura uchaguzi huru, sawa na wa haki
 Utangazaji wa matokeo ya uchaguzi bila kucheleweshwa.
(C) Baada ya Kura
 Kukubali ama kukataa matokeo ya uchaguzi
 Kupinga matokeo ya uchaguzi
1.5 Rushwa na Matumizi ya Rasilimali za Umma Kipindi cha Uchaguzi
Matumizi mabaya ya rasilimali za umma kipindi cha uchaguzi ni dhana pana, kwa kifupi ni
matendo yaliyo kinyume cha sheria yanayotekelezwa na baadhi ya watumishi wa serikali
hasa wale wenye kutaka kuwania nafasi za uongozi, au viongozi wanaotamani kubakia
madarakani.
Mara nyingi matumizi haya yanatumika kwa lengo la kusaidia viongozi kuendelea kushika
dola. Kuna aina mbali mbali ya matumizi ya rasilimali za umma katika uchaguzi kama;
 Matumizi ya rasilimali watu
 Matumizi ya vyombo vya habari vya umma
 Matumizi ya vyombo vya usafiri vya umma
 Matumizi ya fedha za umma
 Matumizi ya mali nyigne za umma
AZAKI zinakemea matumizi mabaya ya rasilimali za umma hasa kipindi cha uchaguzi ikiwa
na lengo tu la kusaidia kiongozi au chama fulani kwa kuwa hii ni kinyume na misingi ya
kidemokrasia na inaweza kuwa kiashiria kimoja wapo cha uchaguzi usio na usawa na wa
haki. Pia tunakemea matumizi ya hongo na rushwa kipindi cha uchaguzi hasa vipindi kura za
maoni ndani ya vyama na baadaye uchaguzi mkuu.
Matumizi ya rasilimali za umma lazima yafuate misingi ya kisheria, na usawa kati ya vyama
vyote vya siasa katika kampeni. Mfano matumizi ya vyombo vya habari vya umma ni vyema
vitumike kwa haki.
13
SURA YA PILI
TANZANIA TUITAKAYO
2.0 Tanzania Tuitakayo
ama sehemu ya kutambua na kuonyesha mchango wetu muhimu kwa maendeleo
ya Taifa, sisi wana AZAKI tumeona ni vyema tukatumia fursa hii ya uchaguzi
mkuu kuwakumbusha wanasiasa mambo ya msingi ambayo tungependa wayape
kipaumbele pindi watakapochaguliwa.
Kwa ujumla, tunapenda kuona Tanzania yenye kuzingatia utawala wa katiba na
sheria, kuheshimu haki za binadamu, ulinzi imara wa rasilimali za nchi,
watanzania wenye kupata huduma bora za kijamii, taifa lenye kujali uwajibikaji na
ushirikishwaji wa wananchi katika mambo ya msingi, pia tungependa kuwa na Tanzania
isiyokumbatia ufisadi na yenye maendeleo ya kiuchumi ili kutoa ajira na kumaliza umaskini
wa watu wake. Sura hii itaeleza kwa kina Tanzania tunayoitaka baaada ya uchaguzi mkuu
tarehe 25 /10/2015.
2.1 Mgawanyo wa Madaraka Utawala wa Katiba na Sheria
Tanzania kwa muda mrefu sasa imekuwa na changamoto kubwa kuhusu utawala wenye
kufuata misingi ya sheria na mgawanyo wa madaraka. Utendaji wa viongozi wengi wa
serikali hasa wanapotekeleza majukumu yao ya kiutawala umekuwa wa kutokuzingatia
Katiba, sheria za nchi na wenye kukiuka haki za binadamu. Hali hii ya kutokutii na
kuheshimu sheria za nchi si tu imekuwa ikijitokeza kwa viongozi bali hata kwa wananchi
wenyewe.
2.1.1 Utawala wa Sheria
Utawala wa sheria maana yake ni kuwa raia na viongozi wanaotii na kuheshimu sheria.
Sheria zote zinapaswa kutekelezwa na kupitishwa kwa uwazi na ushirikishwaji wa wananchi
wote wanaoathiriwa na sheria husika na pia kuhakikisha kunakuwepo na matumizi sahihi ya
sheria husika kwa vyombo vyenye jukumu la kutekeleza sheria hizo. Aidha hauna budi
kuzingatia nguzo kuu tatu za utawala wa Sheria amabazo ni; Uhalali, Demokrasia na Haki
za Binadamu.
Tamko Kuhusu Utawala wa Sheria
K
14
Ili tuweze kuwa na Tanzania yenye kuheshimu utawala wa sheria, mtu mwenye kuutaka
uongozi anapaswa kuwahakikishia watanzania kuwa kutakuwa na Taifa lenye kuuzingatia
utawala wa Katiba na Sheria.
oTunahitaji Taifa ambalo Serikali na watendaji wake pamoja na mtu mmoja mmoja na
taasisi binafsi wanawajibika na kufanya maamuzi kwa mujibu wa sheria.
o Kuwepo na sheria nzuri, zinazojulikana na wote, zenye kuzingatia misingi ya haki,
usawa na usalama wa watu na mali zao. Sheria lazima ziwe wazi vya kutosha kwa
sababu watu hawawezi kutii sheria ikiwa hawazielewi sheria hizo.
oTunahitaji Taifa ambalo mchakato wa upatikanaji wa sheria na sera mbalimbali
utazingatia uwazi na ushirikishwaji wa jamii na makundi mbalimbali ya raia nchini.
oTunahitaji mfumo wa utoaji haki ambao ni huru, imara na wenye kuzingatia weledi,
muda na usawa mbele ya sheria.
oTunahitaji Viongozi ambao watawahakikisha watanzania wanapata katiba bora yenye
kuzingatia maoni ya wananchi, uwajibikaji, utawala bora, mgawanyo wa madaraka
na haki za binadamu.
o Tunahitaji kuzingatia misingi bora ya Katiba hususani mgawanyo wa madaraka.
2. 1.2 Mgawanyo wa Madaraka
Serikali ya Tanzania haina mgawanyo sahihi wa madaraka. Tumeona mihimili mikuu ya dola
hususan Bunge, Mahakama na Serikali vikiingiliana katika utendaji wake wa kila siku na
wakati mwingine mhimili mmoja kukimbia majukumu yake kwa kisingizio cha kuepusha
mgongano na mhimili mwingine.Utawala wa sheria unahitaji kuwa mihimili mikuu ya nchi,
yaani serikali, bunge na mahakama inatenganishwa na haiingiliani katika utendaji kazi.
Kutenganishwa huko kunalenga pia kuzuia watendaji katika chombo kimoja kuwa na
majukumu katika chombo kingine. Kwa mfano, Mbunge kuwa waziri na kushiriki vikao vya
serikali katika baraza la mawaziri.
Dhana ya mgawanyo wa madaraka inaeleza kuwa mamlaka ya Serikali ni utendaji; mamlaka
ya Bunge ni kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma; na mamlaka ya
Mahakama ni kutafsiri sheria na kutoa haki. Hapa Tanzania dhana hii inatajwa kwenye Ibara
ya 4(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Tamko kuhusu Mgawanyo wa Madaraka
o Tunahitaji viongozi watakaohakikisha hakutakuwa na muingiliano wa kimadaraka toka
mhimili mmoja hadi mwingine. Mathalani, Serikali kutotawala, kuingilia ama kufanya
15
kazi za mhimili mwingine kama Bunge na Mahakama. Lengo la mgawanyo wa
madaraka ni kuongeza ufanisi na kuleta uwajibikaji wa mihimili ya dola.
o Tungependa Tanzania ambayo mawaziri hawatatokani na wabunge ili kujenga vizuri
dhana ya mgawanyo wa madaraka na uwajibikaji. Ili kuboresha vizuri majukumu ya
kila mhimili kusimamia na kuwajibisha mhimili mwingine ni vyema bunge likawa huru
kwa kutokuwa na mawaziri ili kulipa nguvu ya kuwawajibisha mawaziri pale
wanaposhindwa kutekeleza majukumu yao kulingana na katiba na sheria za nchi.
o Uwepo wa vyombo huru vya utoaji haki hasa mahakama na Tume ya Haki za
Binadamu na Tume za Uchaguzi.
o Tanzania yenye mfumo wa uongozi ambao hautoi mwanya kwa watumishi wa umma
kushika nafasi za kisiasa.
o Tanzania yenye mfumo wa uongozi ambao hutenganisha shughuli binafsi za kibiashara
na uongozi wa umma ili kuepuka mgongano wa kimaslahi.
o Serikali inayoingia madarakani ipunguze mrundikano wa madaraka kwa watendaji
wake. Endapo mtu atakuwa Mbunge asiwe mkuu wa mkoa/wilaya wala Mjumbe
kwenye Bodi za Mashirika ya umma,
2.2 Haki za Binadamu
Mojawapo ya misingi mikubwa ya utawala bora na wa sheria ni kuheshimiwa na kulindwa
kwa haki za binadamu. Ili Taifa lionekana kuwa linazingatia misingi ya utawala bora na
utawala wa sheria ni muhimu kuheshimu na kulinda haki za binadamu.
Haki za Binadamu ni haki za msingi ambazo mwanadamu yeyote yule bila kujali rangi, umri,
ulemavu, jinsia, wadhifa, taifa wala kabila anakuwa nazo kama binadamu. Haki za binadamu
kama zilivyoainishwa katika Tamko la Haki za Binadamu la mwaka 1948 zimegawanywa
katika makundi mbali mbali kama vile haki za kiraia na kisiasa, haki za kijamii, kiuchumi na
kiutamaduni haki za pamoja na haki za makundi mbalimbali.
Hali ya haki za binadamu hapa nchini Tanzania imekuwa siyo ya kuridhisha ingawa kuna
maeneo tumeanza kuona mabadiliko madogo madogo. Bado Taifa linakosa uhuru wa
kutosha wa maoni na vyombo vya habari kutokana na sababu mbalimbali hususan uwepo wa
sheria kandamizi na zinazozuia uhuru stahiki katika tasnia ya habari. Vile vile, wananchi
wameendelea kujichukulia sheria mikononi ikiwemokuua watu wanaosadikiwa kuwa
16
vibaka,kuvamia vituo vya polisi na mauaji ya watu wenye ualbino. Pia kumekuwepo na
mazingira magumu ya uhuru wa asasi za kiraia na vyama vya kisiasa kufanya majukumu yao
kwa maendeleo ya taifa.
Tamko Kuhusu Haki za Binadamu
(i) Uhuru na Haki za Kiraia
Tunahitaji viongozi watakaozingatia na kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa na serikali
na vyombo vyake kwa mujibu wa sheria, katiba na mikataba ya kimataifa ya haki za
binadamu. Haki hizi ni rahisi sana kutekelezwa na kulindwa endapo tutapata viongozi wenye
nia thabiti.
oSerikali inapaswa kukomesha watu kukamatwa kiholela, kuwekwa kuzuizini na
kuteswa.
o Haki ya Kuishi imekuwa ikivunjwa sana hapa Tanzania, hivyo tunapenda kuona
Tanzania ikipata viongozi wenye kujali na kulinda haki ya kuishi ikiwemo juhudi za
kuondoa adhabu ya kifo.
oTunapenda pia kuona baada ya uchaguzi Tanzania yenye kuzingatia uhuru wa kutoa
maoni, kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari na kupata habari. Katika
kufanikisha hili viongozi watamke kuwa watatoa fursa ya kuzirekebisha ama
kuzifuta sheria zote zinazopokonya uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa
kujieleza na haki ya kupata habari.
oTunahitaji tupate viongozi watakaoweza kudhibiti wimbi la mauaji kwa imani za
kishirikina nchini hususani mauaji ya watu wenye ualbino, wanawake na vikongwe.
oTunategemea kuwa na Taifa lenye kulinda usalama wa watetezi wa haki za binadamu
pamoja na waandishi wa habari wanapokuwa katika majukumu yao.
o Usawa mbele ya sheria ni moja ya haki za msingi kwa kila mtanzania hivyo
tunategemea kuwa na Taifa litakalozingatia utoaji wa haki sawa kwa makundi yote.
(ii) Haki za Kisiasa
Haki za Kisiasa ni haki za msingi katika kutoa fursa kwa wananchi kushiriki katika shughuli
za umma na utawala wa nchi. Kila raia ana uhuru wa kushiriki ipasavyo katika serikali ya
nchi yake moja kwa moja au kupitia wawakilishi wake. Ibara ya 8 na 21 za Katiba
zinasisitiza kuwa mamlaka ya nchi yatatoka kwa wananchi na wananchi wana haki ya
kuchagua na kuchaguliwa.
17
Tamko kuhusu haki za Kisiasa
o Haki ya Kujumuika pamoja na raia wengine ni mojawapo ya haki za msingi kwa
raia wa Taifa lolote lile. Tunawataka viongozi wanaohitaji ridhaa ya kuongoza
Taifa hili kuhakikisha haki hii ya kujumuika na kufanya maandamano inalindwa
na kuheshimiwa.
o Kumekuwa na vikwazo katika kusajili na kuendesha vyama vya kiraia na kisiasa
hapa nchini. Viongozi wote wenye kutaka ridhaa ya watanzania wanapaswa
kuhakikisha kuwa wataweka mazingira rafiki katika kusajili na kuendesha
vyama vya kiraia na kisiasa hapa nchini.
o Wananchi wana haki ya kushiriki katika utawala wa nchi yao. Tunahitaji Taifa
litakalotoa mazingira ya uhuru na ushirikishwaji kwa wananchi katika utawala
wa nchi. Ili kufanikisha hili, inabidi kuwepo mfumo wa siasa unaotoa fursa
sawa kwa wananchi wote na makundi yote ya kisiasa bila ubaguzi au upendeleo.
Pia, ili kuwa na uchaguzi huru na wahaki tunategemea viongozi
watakaochaguliwa waweke mazingira sawa na wezeshi kwa wananchi kushiriki
utawala wa nchi yao. Mathalani kuhakikisha nafasi ya mwananchi kugombea
kama mgombea huru inakuwepo.
o Katiba mpya imekuwa ni kilio cha Watanzania kwa muda mrefu. Kwa msingi
huo tunatoa wito kwa serikali itakayoingia madarakani iwahakikishie wananchi
kuwa itapitisha Katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi.
(iii) Haki za Kiuchumi
Haki za kiuchumi mara nyingi hazipewi sana kipaumbele na serikali yetu na zimekuwa
zikiwekwa katika sehemu ya malengo muhimu ya serikali kwenye katiba, hali inayoondoa
uwezo wa mahakama kuhoji utekelezwaji wake. Haki hizi ni pamoja na haki ya kufanya kazi
na kupata ujira stahiki, haki ya kujiunga katika mashirikisho na vyama vya wafanyakazi na
waajiri, haki ya kuwa katika hali nzuri kiuchumi, haki ya afya na hifadhi ya jamii na haki ya
kumiliki mali.
Hali ya haki hizi hapa nchini siyo ya kuridhisha kutokana na kwamba bado kuna changamoto
kubwa ya ajira, mazingira magumu ya wafanyakazi, na pia wananchi wamekuwa
wakipokonywa haki ya kumiliki mali kama ardhi, mifugo nakadhalika.
Tamko Kuhusu Haki za Kiuchumi
18
o Kulingana na tamko la haki za binadamu la mwaka 1948, haki zote,
zinategemeana na zinalingana katika umuhimu wake. Hivyo basi serikali
inapaswa kupitisha katiba mpya iliyotokana na maoni ya wananchi inayowapa
wananchi uwezo wa kuhoji utekelezwaji wa haki hizi za kiuchumi kama ilivyo
kwa haki za kiraia na kisiasa.
o Serikali inapaswa kuhakikisha inaweka sera, mpango mkakati na vipaumbele
vinavyotekelezeka kuhusu kunyanyua hali ya uchumi kwa wananchi wasio na
ajira hususani kutengeneza mazingira rafiki ya ajira kwa sekta rasmi na wale
wanaojishughulisha kwenye ajira zisizo katika mfumo rasmi, ikiwemo kilimo,
uvuvi na ufugaji.
o Serikali inapaswa kuhakikisha Sheria za ardhi zinazohitaji wananchi
kushirikishwa pale ardhi inapotwaliwa na serikali kwa ajili ya shughuli za
maendeleo na uwekezaji zinatekelezwa.
o Kuwepo na fidia stahiki na ya wakati kulingana na bei ya soko baada ya ardhi
kutwaliwa kwa mujibu sheria.
2.3 Haki za Makundi Maalumu
Haki za makundi maalum ni haki zote zinazojumuisha haki zote za binadamu katika makundi
mbalimbali ya watu wanaotakiwa kupewa uangalizi maalum kwa sababu ya hali ya mazingira
magumu wanayokutana nayo katika jamii. Makundi haya ni kama vile watoto, watu wenye
ulemavu, wakimbizi, wazee, wanawake na makundi mengine madogo madogo katika jamii.
Kwa kuwa haki za watu walio katika makundi haya zimeainishwa katika haki za binadamu,
kumekuwepo na usahaulifu wa mamlaka husika na wananchi kwa ujumla kuwa makundi
haya yanahitaji uangalizi maalum kulingana na mazingira wanayokutana nayo katika maisha.
Mathalani, mauaji ya watu wenye ualbino nchini, sheria kandamizi dhidi ya wanawake na
watoto na pia ukosefu wa hifadhi ya jamii kwa wazee na makundi mengine ya pembezoni.
Tamko Kuhusu haki za makundi maalum
o Serikali inayoingia madarakani ihakikishe inapitisha katiba mpya iliyotokana na maoni
ya wananchi inayoainisha haki za makundi maalum na wajibu wa serikali na jamii
nzima kuhusu makundi hayo maalum.
o Utekelezaji thabiti wa mikataba mbalimbali ya haki za binadamu ambayo Tanzania ni
nchi mwanachama iliyo mahususi kwa ajili ya watoto, wazee, wakimbizi, watu wenye
19
ulemavu, wanawake, vijana na makundi ya pembezoni kama vile wafugaji na
waaokota matunda.
o Serikali kupitisha sera na sheria madhubuti inayowalinda watu wenye ulemavu na
isiyo ya kibaguzi pamoja na kuhimiza na kuweka miundo mbinu iliyo rafiki kwa watu
wenye ulemavu wote kufurahia haki zao za msingi za kikatiba.
o Kuondoa au kurekebisha sheria zote na sera kandamizi dhidi ya wanawake na watoto.
o Kuahakikisha jamii za makundi madogomadogo hasa zilizo pembezoni mwa nchi na
zilizosahaulika zinalindwa na zinapewa fursa ya kunufaika na rasilimali za nchi.
o Serikiali ihakikishe inatekeleza sera ya wazee kwa kutunga sheria itakayosimamia na
kulinda haki zote za msingi za wazee.
o Serikali ihakikishe inaweka mazingira mazuri ya wafugaji asilia na kutumia rasilimali
za nchi ili kupunguza migogoro ya mara kwa mara na wakulima.
2.4 Ulinzi wa Rasilimali Muhimu za Nchi na Haki ya Maendeleo
Haki ya ulinzi na hifadhi ya rasilimali muhimu za nchi ni moja kati ya haki muhimu katika
makundi ya haki za binadamu hususan haki za kiuchumi na haki za pamoja. Hivyo basi,
dhana ya utawala wa sheria na haki za binadamu,ni lazima izingatie ulinzi na matumizi ya
rasilimali za nchi kwa maendeleo ya taifa.
Tanzania ni mojawapo ya nchi zilizobarikiwa kuwa na rasilimali ambazo ni ardhi, madini,
gesi asilia, mafuta, bahari, maziwa, mito, wanyama pori na misitu asilia.
Katika miaka ya hivi karibuni ulinzi thabiti wa rasilimali za nchi hususan kwa mamlaka
husika umekosekana nchini hali inayosababisha upotevu na ubadhirifu wa rasilmali za nchi
kwa mfano, uvunaji haramu wa rasilimali misitu na bahari , umilikishwaji wa ardhi ya
wazawa kinyume na sheria pamoja na ujangili wa wanyamapori. Pia tumeona viongozi
wakiingia mikataba ya uwekezaji uvunaji na wa rasilimali isiyo na tija kwa taifa. Tunawataka
viongozi wote wenye kuwania nafasi za uongozi kutamka bila kificho namna
watakavyosimamia na kulinda rasilimali za nchi ili zitumike kwa manufaa ya Taifa na watu
wake.
Tamko Kuhusu ulinzi wa rasilimali za nchi
o Mamlaka husika katika serikali itakayoingia madarakani zizingatie na kutekeleza
mikataba ya kimataifa ambayo Tanzania ni mshirika inayoelezea haki ya ulinzi wa
rasilimali kwa manufaa ya wananchi wote na wananchi kufaidi rasilimali muhimu za
nchi,kama ilivyo ainishwa kwenye ibara ya 21 ibara ndogo ya 1 ya mkataba wa Afrika wa
haki za binadamu na watu.
20
o Kuwapa wananchi mamlaka ya kikatiba ya kushitaki serikali mahakamani pale viongozi
wanaposhindwa kusimamia ipasavyo rasilimali za nchi.
o Sheria zote zisizolinda rasilimali muhimu au zinazotoa mwanya kwa rasilimali za nchi
kutumika bila kumnufaisha mwananchi zifutwe au kurekebishwa.
o Serikali ijayo isimamie vizuri uvunaji, matumizi na mgawanyo sawa wa rasilimali za
nchi ili kuepuka migogoro baina ya wawekazaji na wananchi pamoja na migogoro ya
wenyewe kwa wenyewe kama vile migogoro ya wakulima na wafugaji.
o Kuwepo na uwazi wa mapato, matumizi na mikataba inayohusu uwekezaji kwenye
rasilimali za nchi kama madini, gesi, mafuta,ardhi, misitu na wanyama pori.
o Mamlaka za nchi zizingatie,kutekeleza na kusisitiza juu ya matumizi mbadala ya nishati
kama gesi ili kunusuru uhai wa misitu asilia na kuepusha hali ya jangwa nchini. Kwa
mfano, gesi asilia iliyovumbuliwa Mtwara itumike kwa manufaa ya wananchi wote na sio
kunufaisha wawekezaji pekee.
2.4 Nafasi na Haki za Asasi za Kiraia
Asasi za Kiraia zimekuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa. AZAKI zimekuwa
mstari wa mbele kutetea haki na maslahi ya watanzania wote. Mara kwa mara , baadhi ya
viongozi wa taifa hili wamekuwa hawathamini mchango na kazi za AZAKI hadi kuzipa
majina mbalimbali kwa lengo la kuzichafua. Asasi za Kiraia hazipewi kipaumbele kama
wadau muhimu wa maendeleo katika Taifa hili. Uhuru wa AZAKI kufanya kazi zao
umekuwa pia ukipata vikwazo vya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa sheria
kandamizi na vizuizi vya kufanya miradi mbalimbali ya maendeleo, ulinzi wa haki za
binadamu, utawala bora na uwajibikaji.
Tamko Kuhusu Nafasi ya AZAKI
o Tunataka viongozi watakaochaguliwa wazingatie umuhimu wa kutambua na kulinda
nafasi ya AZAKI kama wabia muhimu wa maendeleo na utawala bora wenye
kuzingatia sheria katika Taifa.
o Wawe tayari kufanyia marekebisho au kuondoa kabisa sheria mbalimbali
zinazokandamiza uhuru wa AZAKI na watetezi wa haki za binadamu hapa nchini.
o Kukemea baadhi ya viongozi wanaotumia nyadhifa zao kukandamiza na kuzuia
utekelezaji wa kazi za AZAKI katika maeneo yao.
21
o Tunataka viongozi watakaoshirikisha AZAKI katika mipango mbalimbali ya
maendeleo na kuthamini michango ya AZAKI kwa ustawi wa jamii na Taifa.
o Viongozi watakaotoa uwakilishi wa AZAKI katika vyombo vya maamuzi kama Bunge
bila kupitia chama chochote cha siasa. Mfano Rais kutumia madaraka yake ya uteuzi
wa wabunge kumteua mwakilishi wa AZAKI asiyefungamana na chama chochote.
2.5 Huduma Za Kijamii
Huduma za jamii ni haki za msingi katika kujenga jamii yenye maendeleo endelevu.Kwa
mujibu wa Katiba, serikali inapaswa kuweka mazingira wezeshi kuhakikisha huduma za
kijamii zinapatikana kwa urahisi na kwa watu wote na kwa wakati. Huduma hizi ni kama vile
elimu, afya, maji safi na salama. Kwa miaka zaidi ya hamsini baada ya uhuru hali ya utoaji
wa huduma za msingi za kijamii umekuwa sio wa kuridhisha. Katika kuweka mazingira
wezeshi ya upatikanaji wa huduma hizi nchini, wananchi wote wanapaswa kushirikishwa
katika mipango na maamuzi kuanzia ngazi za chini hadi ngazi za juu.
2.5.1 Upatikanaji wa Huduma ya Elimu kwa Wote
Haki ya elimu ni haki ya msingi ya binadamu na ni haki muhimu kwa maendeleo. Haki hii
inahamasisha uhuru na uwezo wa mtu binafsi katika kujiletea maendeleo. Bado
miundombinu ya shule zetu za msingi, sekondari na vyuo hairuhusu upatikanaji wa elimu
bora na endelevu kwa mustakabali wa Taifa. Ubora wa elimu hapa nchini kwa ngazi zote
umekuwa ukishuka kutokana na sababu mbalimbali zikiwepo ukosefu wa walimu wenye sifa
na wakutosha, miundo mbinu mibovu, ukosefu wa vitabu vya ziada na kiada, vifaa vya
kufundishia na mazingira magumu ya kazi na uratibu na usimamizi mbovu wa sekta ya
elimu.
Tamko Kuhusu Elimu
o Tunahitaji viongozi na serikali itakayo kuja na Dira ya Elimu na kuweka mikakati
endelevu ya kuboresha kiwango cha elimu kwa manufaa ya watanzania wote.
o Viongozi waweke mazingira bora ya kutolea elimu inayozingatia mahitaji ya makundi
maalum na watoto wenye mahitaji maalum. Kuhakikisha watoto wote wenye umri wa
kwenda shule wanakwenda kwa kupiga vita ajira kwa watoto wenye umri wa kuwa
shule.
o Tunamtaka kiongozi atakayejali na kuboresha mishahara na maslahi ya walimu na
kuondoa kabisa tatizo la upungufu wa walimu kwa shule za sekondari na msingi.
22
o Kiongozi atakayechaguliwa asimamie na kuondoa tofauti kubwa za ubora kati ya
shule za serikali na zile za binafsi.
o Tunawatakaviongozi watakaochanguliwa kufuta sheria za kibaguzi zinazominya fursa
ya mtoto wa kike kupata elimu, baadhi ya sheria hizo ni pamoja na zinazochangia
mtoto wa kike kuolewa akiwa na umri mdogo.
o Tunahitaji kiongozi atakaye hakikisha kuwepo kwa usawa wa kijinsia katika sekta ya
elimu.
o Viongozi watakaoingia madarakani wahakikishe kunakuwepo na miundo mbinu rafiki
ya kujifunzia kwa watu wote ikiwemo watu wenye ulemavu.
2.5.2 Huduma za Afya
Haki ya kiwango stahiki cha maisha inatambuliwa chini ya Ibara ya 25 (1) ya Tamko la
Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu, ikiwepo; “Kila mtu ana haki ya kiwango cha maisha
kinachokidhi afya na ustawi wake na familia yake, pamoja na chakula, mavazi, makazi na
matibabu na huduma muhimu za jamii……..”
Hali halisi ya upatikanaji wa huduma za afya nchini Tanzania hairidhishi hivyo kuathiri haki
ya kuishi. Bajeti ya Taifa kwa kipindi cha miaka zaidi ya 10 haijakidhi azimio la Abuja la
kutenga kiasi cha asilimia 15 ya fedha za ndani kwa ajili ya bajeti ya afya. Pamoja na kuwa
na mipango mbalimbali ya utekelezaji, uzoefu umeonyesha kuwa fedha zinazotengwa na
serikali hazifiki kwa wakati ili ziweze kutekeleza majukumu mbalimbali ya afya.
Hivyo kutokana na hali hiyo sekta ya afya imekuwa na hali mbaya kwa kukosa watumishi
wa kutosha, vifaa tiba, miundombinu mibovu na mishahara midogo.
Tamko kuhusu huduma za afya
o Tunataka serikali itakayoingia madarakani kuondoa tatizo la kulipishwa fedha za
matibabu wanawake wanaojifungua katika zahanati za kata na hosiptali za umma.
Tungetaka kuona serikali itakayoingia madarakani ikitenga fedha za kutosha kwenye
bajeti yake kwa ajili ya sekta ya afya ili kuboresha huduma za afya iwez kufikia au
kuzidi aslimia 15 zilizopendekezwa na Azimio la Abuja..
o Tunataka kuona watu wanaoishi na ulemavu, virusi vya UKIMWI, watoto chini ya
umri wa miaka mitano nao wapatiwe huduma za afya nzuri na za kutosha bure kwa
hospitali zote.
o Tunahitaji kuona uongozi utakaohakikisha kuwa magonjwa kama saratani na
shinikizo la damu yaingizwe kwenye mfumo wa kupata matibabu kwa njia ya
Mfuko wa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii (NHIF na CHF ).
23
o Tunataka serikali ijayo iboreshe utaratibu wa wazee na watoto kupata matibabu ya
bure.
o Watanzania wanahitaji uongozi utakao okoa maisha ya wananchi masikini kwa
kupeleka wataalamu wa kutosha wa afya maeneo yote hasa ya vijijini.
o Serikali itakayoingia madarakani ihakikishe inajenga nyumba za wafanyakazi kwenye
zahanati zote nchini ili kusogeza huduma karibu na wananchi.
o Tunahitaji kuona viongozi watakaohakikisha watu wenye ualibino wanapata vifaa vya
kujikinga na magonjwa na mionzi kama vile mafuta maalum ya ngozi na miwani ya
jua.
o Tunahitaji kuona utaratibu wa huduma za matibabu nje ya nchi unakuwa wazi na
unatolewa bila upendeleo. Pia serikali iboreshe huduma za afya hapa nchini ili
kupunguza gharama za matibabu nje ya nchi.
o Tunahitaji viongozi watakaolinda haki za mlaji wa madawa na vyakula dhidi ya
madawa na vyakula vyenye madhara kiafya na kiwango duni.
2.5.3 Huduma za Maji Safi na Salama
Huduma ya maji ni moja wapo ya huduma za msingi kwa maisha ya binadamu kwa kuwa
maji ni uhai. Sera ya maji ya mwaka 2002 inaeleza kuwa madhumuni ya jumla ya sera
kuhusu utoaji wa huduma ya maji ni kuboresha afya ya jamii na kusaidia kuondoa umaskini
vijijini ikiwa ni pamoja na kuboresha upatikanaji wa maji safi salama na yakutosha.Hata
hivyo hali halisi ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa mijini na vijijini
imekuwa tatizo sugu.
Tamko kuhusu huduma za maji
o Tunataka kuona viongozi watakaochaguliwa wakihakikisha kuwa tatizo la wanawake
wa mijini na vijijini kutembea umbali mkubwa kutafuta maji linapatiwa ufumbuzi.
o Maji yawe ni kipaumbele cha serikali ijayo na kuhakikisha bajeti ya maji inaongezwa
ili kukidhi mahitaji.
o Maji yasiwe bidhaa Kama ilivyo sasa, iwe ni huduma ya msingi na serikali ihakikishe
wananchi wote wanaipata bila tatizo.
o Serikali ihakikishe inasimamia vyanzo vya maji na utunzaji wa mazingira kwa kutoa
elimu
24
2.6 Ushiriki na Ushirikishwaji wa Wanachi katika Maamuzi
Kuna changamoto mbalimbali zinazokabili utendaji wa mamlaka ya serikali za mitaa hadi
serikali kuu. Hadi sasa mamlaka ya wananchi imeporwa na haijulikani ipo wapi. Haieleweki
ni namna gani wanashiriki katika maamuzi na katika shughuli za maendeleo na ukuaji wa
uchumi wa nchi, huduma za Jamii na maisha yao kwa ujumla.
Tanzania ya leo, inahitaji kiongozi atakayesimamia na kuweka mikakati thabiti ya
uanzilishwaji na utekelezwaji wa mpango wa uboreshaji wa mfumo wa serikali za mitaa
ulioanza mwaka 1998 ambao ulilenga kupeleka madaraka kwa wananchi. Miradi mbalimbali
ya maendeleo imekosa ushiriki kamilifu wa wananchi katika hatua za awali za uibuaji na
usimamizi.
Tamko kuhusu ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi:
o Serikali itakayoingia madarakani ihakikishe inaboresha sheria za serikali za mitaa
ili ziweze kuwawajibisha viongozi wa vijiji/mitaa ambao hawashirikishi wananchi
kwenye zoezi la kuibua, kupanga na kusimamia miradi katika maeneo yao
o Viongozi watakaoingia madarakani waweke utaratibu utakaozibana serikali za
mitaa/serikali kuu kuheshimu maamuzi ya vikao halali vya serikali za mitaa/vijiji
vilivyobainisha vipaumbele vya wananchi na hivyo ndivyo vipewe fedha kwa
utekelezaji
o Miongozo ya usimamizi wa rasilimali za umma iliyotolewa na TAMISEMI
isimamiwe na kutekelezwa kikamilifu ili wananchi washiriki kuwawajibisha
viongozi wabadhirifu wa rasilimali za umma.
o Kuhakikisha wananchi kuanzia ngazi ya vijiji/mitaa kupitia serikali zao
wanashiriki ipasavyo katika kutunga sera za nchi badala ya kuwa watekelezaji tu.
o Serikali itakayoingia madarakani iwaelimishe wanachi kuhusu ulipaji kodi na
ihakikishe inakusanya kodi na kutumia mapato ya kodi hizo kwa manufaa ya
wananchi
2.7 Usawa wa Kijinsia
Dhana ya usawa wa jinsia inatumika pale ambapo jamii imeweza kuondoa pengo
lililojengeka katika kufikia, kumiliki na kufaidi rasilimali zinazoshikika na zisizoshikika
katika jamii husika. Kimantiki usawa wa jinsia ni hali ya maisha isiyojengeka katika kubagua
mwanamke au mwanaume kutokana na jinsi au hali yake.
25
Hapa kwetu Tanzania usawa wa jinsia unapanuka kwa kasi ndogo na hivyo kudhoofisha
demokrasia na kuathiri maendeleo yetu hususan vita dhidi ya umaskini. Azimio la Umoja wa
Afrika kupitia Mkataba wa Nyongeza wa Maputo uliagiza nchi wanachama kufanya
marekebisho ya Katiba ili kuwezesha kufikia 50/50 usawa wa kijinsia katika Uongozi
ifikapo mwaka 2015.
Tamko kuhusu usawa wa Kijinsia
o Serikali itakayoingia madarakani ihakikishe inawezesha kufikiwa kwa lengo la
50/50 kwenye nafasi zote za uongozi
o Viongozi watakaochaguliwa wadhibiti mfumo unaoruhusu wenye mali
kuhodhi madaraka ya kisiasa ambao unadhohofisha demokrasia shirikishi,
na kuadhiri ushiriki wa Wanawake na wanaume masikini katika maamuzi ya
uongozi wa taifa lao katika ngazi zote.
o Kuweka utaratibu wa kisheria na kikatiba utakaotoa mwongozo kuwezesha
makundi yote ya jamii kama wanawake, makundi ya pembezoni na wenye
ulemavu wa viungo wanashiriki kikamilifu katika uchaguzi kama wapiga
kura na kama wagombea uongozi wa nyadhifa mbalimbali.
o Kupiga marufuku matumizi ya lugha za kashfa , matusi, udhalilishaji kwenye
chaguzi zote ili makundi yote yaweze kushiriki bila kikwazo.
o Tunataka serikali ambayo itarekebisha au kuondoa kabisa sheria kandamizi
kwa haki za mtoto na mwanamke kama ile sheria ya Ndoa ya 1971.
2.8 Uchumi Endelevu na Ajira
Haki ya kupata ajira ni haki inayotambulika kikatiba, na serikali inalo jukumu la kuhakikisha
kuwa inaweka mazingira safi na rafiki ili kumpa nafasi mwananchi kunufaika na haki hiyo.
Hata hivyo, ajira bado ni changamoto kubwa sana Tanzania. Pamoja na ongezeko la wasomi
nchini, pia ahadi za viongozi mbalimbali wa serikali kuweka mazingira bora ya ajira baada ya
kuingia madarakani, serikali na taasisi za umma zimekuwa hazitoi kipaumbele na kusisitiza
upatikanaji kwa wingi wa ajira na kutokuweka mazingira rafiki ya kujiajiri, hali
inayosababisha hali mbaya ya kiuchumi kwa watanzania wengi hasa vijana.
Kilimo ambacho kinaajiri watanzania zaidi ya asilimia 80 bado hakijaweza kuwakwamua
wananchi walio wengi ambao wameendelea kuishi katika hali isiyoridhisha kiuchumi kwa
kuwa wengi wao ni wakulima wadogo wadogona wamekua wakitumia mbinu na nyenzo duni
zisizo endana na teknolojia ya kilimo cha kisasa. Pamoja na kuwa serikali tangu kupata
26
uhuru imekua na kauli mbiu na mikakati mbali mbali ya kuendeleza na kukuza sekta ya
kilimo kama vile „siasa ni kilimo‟, „kilimo ni uti wa mgongo‟ na pia kwa sasa „kilimo
kwanza‟, bado kauli mbiu hizi hazijaweza kubadilisha hali kwa kuwa hazikutekelezwa
ipasavyo.
Tofauti na kilimo sekta nyingine za uchumi zinazoweza kusaidia kuinua ajira nchini ni utalii,
uvuvi, usafiri, mawasiliano, viwanda na biashara, uchimbaji madini na kadhalika. Kwa
kiwango fulani, baadhi ya sekta kama za usafiri zimeweza kuwaajiri vijana wengi ingawa
bado wanafanya kazi katika mazingira magumu.
Tamko kuhusu ajira na Uchumi
o Tunahitaji kuwa na viongozi wenye mipango na mikakati thabiti na
inayotekelezeka ya kufufua na kuendeleza kilimo cha kisasa na endelevu kwa
kutumia umwagiliaji na nyezo za kiteknolojia za kilimo cha kisasa.
o Inahitajika mikakati ya wazi ya namna viwanda vitakavyoboreshwa nchini kwa
kuanza na viwanda vidogo vidogo vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo
kama vile vya kusindika matunda, ufungaji korosho na senene, ufugaji wa nyuki
na uhifadhi wa madafu na vinginevyo ili kuhakikisha kuwa kilimo kinakuza ajira
na uchumi kwa kusafirisha mazao nje ya nchi.
o Viwanda vilivyokuwa vikizalisha mazao kama vile nguo, nyama, minofu ya
samaki, pamba na vinginevyo vifufuliwe na kuanza kufanya kazi tena.
o Mazingira rafiki ya kujiajiri yatengenezwe ikiwa ni pamoja na kuwawezesha
wananchi kwa kuwapa mitaji, kurahisisha masharti ya kukopa pesa na nyenzo
muhimu, pia kuweka mitaala ya ujasiriamali na kilimo bora cha kisasa katika
mfumo wa elimu nchini kuanzia ngazi za chini hadi vyuoni.
o Kuboresha maslahi ya wafanyakazi na wananchi waliojiajiri katika sekta binafsi
kwa kuwapa motisha..
2.9 Uwazi na Uwajibikaji wa viongozi wa Umma
Ili shughuli za umma ziweze kutekelezwa vema kwa maendeleo ya taifa zima, mazingira ya
kisheria na kiutendaji yanapaswa kuwa shirikishi na wazi. Bila jambo hili, uwajibikaji wa
viongozi na wananchi hautawezekana. Katika nchi yeyote inaofuata misingi ya
kidemokrasia, uwazi na uwajibikaji wa viongozi wa umma na wananchi kwa ujumla ni
nyenzo muhimu sana kwa maendeleo ya nchi.
27
Viongozi wa serikali kutokuwa wawajibikaji na kukithiri kwa usiri wa maamuzi na shughuli
zenye manufaa kwa umma imekuwa ni jambo la kawaida sana nchini. Bunge ambalo ni
mhimili mkuu unaotakiwa kuisimamia na kuiwajibisha serikali kwa mujibu wa Katiba
umekuwa haupewi nafasi ya kushirikishwa katika maamuzi mengi yanayofikiwa na serikali,
hasa mikataba mbalimbali ambayo serikali inaingia kuhusu masuala ya uwekezaji katika
rasilimali za nchi. Hali hii imesababisha kukithiri kwa ufisadi, ubadhirifu na kukasimisha
rasilimali za nchi kwa wageni, hali isiyowanufaisha wananchi na taifa kwa ujumla.
Aidha, kumekuwepo na mtindo wa kupeleka miswada ya sheria bungeni kwa hati ya dharura
kwa masuala muhimu kama uhuru wa habari na haki ya kupata taarifa, na miswaada ya
rasilimali ya gesi na mafuta. Hali hii ni usaliti kwa watanzania. Katika nchi ambayo wananchi
hawako katika mazingira mazuri ya kupata taarifa kwa wakati kama Tanzania, inashangaza
kuwa serikali inafurahia kuendelea kuficha taarifa za msingi za utekelezaji wa shughuli za
umma, sera na sheria muhimu za nchi kwa maendeleo ya taifa la leo na vizazi vijavyo.
Tamko Kuhushu Uwazi na Uwajibikaji
o Tnahitaji viongozi ambao watatetea uwazi na uwajibikaji serikalini na katika mihimili
ya dola. Hii itakuwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa miswada mbalimbali
ilyoandaliwa kama vile ya sheria za haki ya kupata taarifa na uhuru wa habari na
sera zake zitapelekwa bungeni kwa muda mahsusi baada ya maoni ya wananchi.
o Tunataka kuona viongozi wanapitisha na kulinda katiba mpya itokanayo na maoni ya
wananchi.
2.8 Rushwa, Ufisadi na Ubadhirifu wa mali za Umma
Tanzania katika siku za karibuni imeshudia kushamiri kwa tatizo la rushwa, ufisadi na
matumizi mabaya ya mali za umma uliosababisha kudidimiza sana uchumi wa nchi. Rushwa
ni matumizi mabaya ya madaraka au nafasi aliyenayo mtu kwa ajili ya kujinufaisha. Pia,
inahusisha kitendo cha kumpa mtu aidha pesa, hali au mali ili akupe upendeleo fulani. Pia
Taifa linakumbwa na tatizo la ukusanyaji na usimamizi mbovu wa mapato yatokanayo na
kodi.
28
Wakati wa uchaguzi na hata baada ya chaguzi kumekuwepo na vitendo vya rushwa
vilivyokithiri hapa nchini hali inayosababisha ukosekanaji wa haki na kudumaa kwa
maendeleo ya Taifa. Kwa ujumla wake, ufisadi unajumuisha maovu au uharibifu wa namna
yoyote ile ikiwemo matumizi mabaya ya ofisi za umma au binafsi kwa manufaa ya mtu
binafsi au kundi la watu.
Nchini Tanzania, ingawa kuna sheria zinazodhibiti matumizi ya pesa au mali binafsi au ya
umma katika chaguzi, sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa na pia taasisi maalum kwa
ajili ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), utekelezaji wake umekuwa si wa
kuridhisha sana hali inayosababisha kushamiri kwa vitendo vya kifisadi hasa kwa viongozi
wa serikali na umma huku wananchi wakiendelea kuwa mafukara.
Tamko kuhusu Rushwa, Ufisadi na Ubadhirifu wa Mali za Umma
o Tunatakaa kuona sheria za kuzuia na kupambana na rushwa wakati wote
zinatekelezwa kikamilifu na wahusika wanachukuliwa hatua stahiki.
o Tunahitaji kuona uhuru na uwazi wa taasisi za kuzuia na kupambana na rushwa katika
utekelezaji wake wa kazi. Hii ni pamoja na kuweka wazi ripoti za rushwa na ufisadi
nchini.
o Tunataka kuwa na kiongozi mwadilifu, anayechukia rushwa, mwenye mikakati thabiti
ya kuondoa tatizo hili na aliyetayari kuwajibika pale itakapobainika amehusika kwa
namna yoyote ile katika ufisadi.
o Tunataka kuwa na Taifa linaloweza kumaliza rushwa kwenye ukusanyaji wa kodi na
hatimaye kukusanya kodi toka kwa makundi yote hasa makampuni makubwa ya
uwekezaji badala ya kuendelea kumuumiza mtanzania kwa kodi mbalimbali huku
wakitoa misamaa ya kodi kwa makampuni makubwa.

29
SURA YA TATU
WITO KWA WADAU
3.1 Kwa Wananchi
 Wananchi ndio wadau muhimu katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba
25 mwaka huu, hivyo wanapaswa kushiriki kikamilifu katika mikutano yote ya
kampeni kusikiliza sera za wagombea wote wa vyama vya siasa ili wakati wa kupiga
kura wafanye maamuzi sahihi.
 Viongozi wabovu huwekwa madarakani na raia wema ambao huwa hawajitokezi
kupiga kura. Hivyo tunawahimiza wananchi waliojiandikisha wajitokeze kwa wingi
siku ya kupiga kura na kutimiza wajibu wao.
 Aidha wananchi wasikubali kwa hali yoyote kurubuniwa na wanasiasa na kupoteza
haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka. Baada ya serikali ya awamu ya tano
kuapishwa wananchi wawe tayari kushiriki hatua zote za michakato ya maendeleo
badala ya kuwaachia wanasiasa kuamua na kutekeleza wenyewe.
 Ni lazima kufuatilia Kwa karibu ili kuweza kuwawajibisha viongozi na watendaji
wote ambao hawatimizi majukumu na ahadi zao wakati wote.
3.2 Kwa vyama vya siasa
 Vyama vya siasa vinapaswa kuendesha kampeni za kistaarabu zinazoheshimu misingi
ya sheria na siasa za ushindani ambazo zinatambua kuwa kuna kushinda na
kushindwa.
 Kusiwepo na kampeni za vitisho, matusi na ubaguzi wa aina yoyote na badala yake
kuwepo kampeni za kistaarabu zinazoheshimu na zinazozingatia maadili ambayo
vyama vyote vya siasa vimesaini.
 Vyama vihakikishe vinasambaza ilani zao za uchaguzi kwa wingi kwa wananchi. Pia,
chama kitakachoshinda kiunde serikali na kuipa jukumu la kutekeleza ahadi zote
zilizoandikwa kwenye ilani ya chama chao.
3.3 Kwa Wagombea
 Tunawasihi wagombea wajikite kwenye ajenda za wananchi sambamba na ilani za
vyama vyao na kuacha kuwahadaa wananchi kwa ahadi ambazo wanajua hawataweza
kuzitimiza.
30
 Tunawataka wagombea waache tabia ya kutumia pesa kuwahonga wananchi na njia
nyingine zisizostahili kwa lengo la kujipatia madaraka.
3.4 Tume za uchaguzi (NEC/ZEC)
 Tume za uchaguzi zifanye kazi kwa uhuru, kufuata sheria, kusimamia kanuni
walizokubaliana na vyama vya siasa na kujiepusha kwa namna yoyote kukipendelea
chama chochote wakati wote wa mchakato wa uchaguzi.
 Tume zinapaswa kuhakikisha kuwa zimewapa mafunzo ya uhakika maofisa na
wasidizi wa uchaguzi na kuchunguza mienendo yao kabla hawajawakabidhi vituo vya
kazi ili kuepusha makosa yaliojitokeza wakati wa kuandikisha wapiga kura.
 Tume za Uchaguzi zinapaswa kufanya maandalizi mapema, pia kusambaza vitendea
kazi vinavyotakiwa kwa wakati ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza siku ya
upigaji kura.
 Tume zihakikishe kuwa watu wote wenye sifa na kustahili kupiga kura ambao
hawakuandikishwa kupiga kura kwa sababu mbali mbali ikiwemo wanafunzi
wanaandikishwa katika daftari la kudumu la kupiga kura na wanapiga kura.
 Tume zitangaze matokeo sahihi bila ya kuchelewesha ili kuepusha kutokea kwa
vurugu zinazoweza kujitokeza.
3.5 Vyombo vya Ulinzi na Usalama
 Vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi zake kwa uweledi na tahadhari ya
kutowatia hofu wananchi na wapiga kura. Vyombo vya ulinzi visitumie vitisho,
nguvu, na silaha za kivita wakati wa mikutano ya kampeni na siku ya kupiga kura.
 Vyombo vya usalama havipaswi kwa namna yoyote kuegemea upande wowote wa
chama cha siasa bali vitende haki kwa vyama vyote na wananchi wote wakiwemo
wagombea mmoja mmoja na wala visikubali kuyumbishwa na mamlaka yoyote nje ya
sheria inayovipa mamlaka kutekeleza wajibu wao.
 Tunalishauri Jeshi la Wananchi wa Tanzania kutojihusisha na mchakato wa uchaguzi
kuanzia kipindi cha maandalizi, cha kampeni, upigaji kura na baada ya upigaji kura.
3.6 Wadau wa Kimataifa
31
 Wadau wa kimataifa waendelee kuzisaidia serikali zetu kitaalamu na kifedha ili
ziweze kufanikisha mchakato wa uchaguzi huru na wa haki.
 Wadau wa kimataifa waendelee kufanya kazi kwa karibu na Asasi za kiraia ili
kufanikisha utoaji wa elimu ya uraia na mpiga kura kwa wananchi.
 Wadau wa kimataifa wajiepushe kuingilia masuala ya ndani ya vyama vya siasa.
3.7 Watumishi wa serikali
 Watumishi wa serikali wanaogombea nyadhifa mbali mbali za kisiasa wasiruhusu na
wasitumie mali za umma wakati wa michakato yote ndani ya vyama vya siasa na hata
wakati wa uchaguzi mkuu.
 Watumishi wa umma wawe huru wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu na pia
watumie haki yao ya kikatiba kuwachagua viongozi wanaowataka bila ya kupokea
shinikizo na vitisho kutoka kwa mtu yeyote ndani na nje ya serikali.
3.8 Vyombo vya Habari
 Vyombo vya habari na waandishi wa habari wafuate na kuzingatia maadili ya taaluma
yao kwa kuhakikisha taarifa wanazozitoa kwa umma hazipendelei chama au
mgombea yoyote bali zilenge kuchambua sera za vyama na tija yake kwa wananchi.
 Aidha, vyombo vya habari vya umma vinavyoendeshwa kwa kodi za wananchi
vihakikishe kwamba vinawapatia fursa sawa wagombea na vyama vyote vya siasa.
3.9 Viongozi wa Dini
Viongozi wa dini wanapaswa kuhubiri amani kwa wafuasi wao na kujiepusha na kutamka
kauli zenye muelekeo wa kupendelea mgombea au chama fulani kwenye maeneo yao ya
ibada, majukwaani na hadharani. Hata hivyo wanaweza kutoa ushauri au elimu ya uraia kwa
waumini wao na taifa pasipo kuegemea itikadi yoyote.
32
SURA YA NNE
HITIMISHO
isi Asasi za Kiraia tukiwa ni sehemu ya wananchi na wapiga kura, tunatoa ilani hii
iwe ni dira na mwongozo kwa wananchi, wagombea, tume za uchaguzi, vyombo vya
ulinzi na usalama, vyama vya siasa na wadau wengine hapa nchini. Ni imani yetu
kuwa ilani hii itatumika katika kuhakikisha tunakuwa na mchakato wa uchaguzi
ambao ni huru, wa haki na usiokuwa na matumizi ya nguvu, rushwa, hongo na
matumizi mabaya ya fedha na rasilimali za umma. Aidha, tunayo imani pia kuwa,
wagombea, vyombo vya habari, viongozi wa dini na wadau wengine wataepuka
lugha za chuki na kibaguzi na uchochezi wa aina yoyote. Kwa kufanya hivyo, Tanzania
itaweza kupata viongozi wanaoheshimu utu, haki za binadamu na kuwajibika kwa wananchi
ambao ndio msingi kwa wananchi wanaowatumikia kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.