Tume ya Uchaguzi Yatoa Tahadhari kwa Viongozi wa Dini

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji, Damian Lubuva akitoa mada jijini Dar es salaam kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji, Damian Lubuva akitoa mada jijini Dar es salaam kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.

Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na NEC jijini Dar es salaam wakifuatilia mada iliyokuwa zikiendelea.

Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria mkutano ulioandaliwa na NEC jijini Dar es salaam wakifuatilia mada iliyokuwa zikiendelea.

Wanasekretarieti ya maandalizi ya mkutano NEC na wadau mbalimbali na baadhi ya waandishi wakifuatilia mjadala kuhusu wajibu wa viongozi wa dini kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Wanasekretarieti ya maandalizi ya mkutano NEC na wadau mbalimbali na baadhi ya waandishi wakifuatilia mjadala kuhusu wajibu wa viongozi wa dini kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

TUME ya Taifa ya uchaguzi NEC imewaomba viongozi wa dini zote kutumia majukwaa yao kuwaelimisha wapiga kura bila kuonyesha hisia za kuegemea upande wowote wa mgombea ili waweze kufanya maamuzi sahihi wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva kwenye Mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam uliowakutanisha wadau hao wa uchaguzi na kuwakumbusha wajibu wao katika jamii hususani katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu.

Alisema kuwa taasisi za kidini zinaaswa kama walivyo wadau wengine katika kipindi hiki cha uchaguzi kuhubiri amani na kuendelea kutoa elimu kwa watanzania ili zoezi hili liishe kwa amani na kuwaacha watanzania wakiwa na umoja na mshikamano licha ya tofauti za kiimani zilizopo miongoni mwao.

“Tume inawataka, nyinyi viongozi wa dini, mnapotoa mafundisho ya uchaguzi kwa waumini wenu kuhakikisha hamuonyeshi hisia za kuwa upande wa chama chochote cha kisiasa na zaidi kuepuka kushawishi waumini wenu kuegema chama au mgombea fulani,” amesema Jaji Lubuva.

Mmoja wa washiriki wa mkutano huo, Askofu Philemon Phiri wa kanisa la EAGT – Mikocheni -A ameiasa Tume hiyo kusimama katika haki, uhuru na kuhakikisha wanatangaza washindi bila kuonyesha upendeleo ili kuivusha nchi ikiwa salama.

Mshiriki mwingine kutoka Kanisa la Moravian Mchungaji Alamu Kajuna alisema kuwa amani ndiyo tunu kwa kila mwanadamu, hatutegemei vurugu wakati huu wa uchaguzi maana amani inapotoweka wanaoumia ni wananchi wakiwamo waumini wao hivyo wao kama taasisi zinazoshirikiana na wananchi kwa karibu kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi ili tupate viongozi kwa amani

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekutano na viongozi hao na wadau wengine ikiwa zimebaki siku mbili kuanza kwa kampeni hapo Jumamosi ijayo kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao.