TFF Yataja Kiingilio Mpambano Yanga na AZAM FC

Nembo ya Azam FC

Nembo ya Azam FC


MCHEZO wa Ngao ya Hisani ambao ni sehemu ya ufunguzi wa pazi la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) nchini kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC utachezwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salam, ambapo kiingilio cha chini kitakua ni shilingi elfu saba. Fuata link chini kwa taarifa kamili

Mchezo wa Ngao ya Hisani ambao ni sehemu ya ufunguzi wa pazi la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) nchini kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC utachezwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salam, ambapo kiingilio cha chini kitakua ni silingi elfu saba..

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, limetangaza viingilio vya mchezo huo ambao utaanza kutimua vumbi majira ya saa 10 kamili jioni, kuwa ni tsh 7,000 kwa majukaa yenye rangi ya kijani, bluu na rangi ya chingwa, VIP B & C tsh 20,000 na VIP A tsh 30,000.

Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya mchezo jumamosi asubuhi saa 2 kamili katika viunga vya maeneo ya uwanja wa Taifa jijini Dar es slaam.

Mchezo huo wa Ngao ya Jamii utachezeshwa na mwamuzi Israel Mjuni Nkongo, (Dsm), akisaidiwa na Samwel Hudson Mpenzu (Arusha), Josephat Daud Bulali (Tanga), mwamuzi wa akiba Hashim Abdallah (Dsm) wakati kamisaa wa mchezo huo ni Deogratius Rwechungura kutoka mkoani Mara.

Wakati huo huo; ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) imetoka leo ambapo jumla ya timu 16 zinashiriki ligi hiyo itakayoanza kutimua vumbi Septemba 12 katika viwanja tofauti nchini na kumalizika Mei 7, 2016.

TFF inavisisitiza vilabu kukamilisha usajili wao wa wachezaji na viongozi kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo la usjaili kesho alhamisi Agosti 20, 2015. Baada ya kufungwa kwa usajili huo hakutakua na muda tena wa nyongeza. Fuata link chini kwa taarifa kamili.

Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) imetoka leo ambapo jumla ya timu 16 zinashiriki ligi hiyo itakayoanza kutimua vumbi Septemba 12 katika viwanja tofauti nchini na kumalizika Mei 7, 2016.

TFF inavisisitiza vilabu kukamilisha usajili wao wa wachezaji na viongozi kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo la usjaili kesho alhamisi Agosti 20, 2015. Baada ya kufungwa kwa usajili huo hakutakua na muda tena wa nyongeza.

Kwa klabu ambayo haitawasilisha malipo ya ada ya mchezaji wa kigeni ya dola elfu mbili (U$D 2000) mchezaji huyo hataruhusiwa kucheza kwenye ligi hadi malipo hayo yatakapofanyika.

Michezo saba itachezwa siku ya ufunguzi jumamosi katika viwanja tofauti ambapo Ndanda Vs Mgambo Shooting (Nang’wanda – Mtwara), African Sports Vs Simba SC (Mkwakwani – Tanga), Majimaji Vs JKT Ruvu (Majimaji – Songea), Azam FC Vs Tanzania (Azam Complex – Dsm), Stand United Vs Mtibwa Sugar (Kambarage – Shinyanga), Toto Africans Vs Mwadui (CCM Kirumba – Mwanza), na siku ya jumapili Young Africans Vs Coastal Union (Taifa – Dar es salaam).