CCM Waweka Hadharani Kikosi cha Kampeni Uchaguzi Mkuu

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Moses Nnauye.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Moses Nnauye.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa Agosti 17, 2015 imekutana katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam na kuteuwa timu ya kampeni ya chama hicho.

Kikao hicho cha kamati kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete pia kimekamilisha kazi ya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo mawili ya Singida Mashariki na Kiteto na kuyaweka hadharani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Moses Nnauye wagombea ubunge walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo hayo ni pamoja na Jonathan Njau (Singida Mashariki) na Emmanuel Papian John (Kiteto).

“Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Kamati ya Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. Wajumbe wa Kamati hiyo ni kama ifuatavyo;-

“…Ndugu Abdulrahman Kinana (Mwenyekiti), Ndugu Rajab Luhwavi (Makamu Mwenyekiti – Bara), Ndugu Vuai Ali Vuai (Makamu Mwenyekiti – Z’bar), Ndugu Sofia Simba, Ndugu Mohamed Seif Khatib, Ndugu Asha-Rose Migiro, Ndugu Samwel Sitta na Ndugu Nape Nnauye.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni pamoja na Ndugu Mwigulu Nchemba, Ndugu Harrison Mwakyembe, Ndugu January Makamba, Ndugu Amina Makillagi, Ndugu Christopher Ole Sendeka, Ndugu Stephen Wasira, Ndugu Abdallah Bulembo, Ndugu Hadija Aboud, Ndugu Mohamed Aboud, Ndugu Lazaro Nyalandu, Ndugu Issa Haji Ussi, Ndugu Waride Bakari Jabu, na Ndugu Mahmoud Thabit Kombo.

Wengine ni pamoja na Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Ndugu Maua Daftari, Ndugu Stephen Masele, Ndugu Pindi Chana, Ndugu Shaka Shaka, Ndugu Makongoro Nyerere, Ndugu Bernard Membe, Ndugu Sadifa Juma Khamis, Ndugu Antony Diallo, Ndugu Livingston Lusinde na Ndugu Ummy Mwalimu.