SERIKALI ya Sudan Kusini imekataa kusaini mkataba uliotarajiwa kuleta amani na kumaliza mapigano yaliyodumu nchini humo kwa zaidi ya miezi ishirini. Hata hivyo waasi na makundi ya upinzani wamesaini kwa upande wao, ilhali Rais Salva Kiir ajaridhia kutia saini mkataba huo.
Serikali imeomba kuongezewa siku kumi na tano zaidi kushauriana juu ya mapendekezo hayo. Waziri kutoka Uingereza anayesimamia maswala ya Afrika ameitaka serikali ya Sudan Kusini kutia sahihi mkataba huo haraka iwezekanavyo. Alisema kuwa watu hawafai kusheherekea hadi pale rais Kiir atakapotia sahihi mkataba huo.
-BBC