ActionAid Yakutanisha Wadau Kujadili Malengo Mapya ya Milenia

Wakili wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Honestus Michael Kulaya akiwasilisha mada katika semina iliyoandaliwa na taasisi ya Landesa.

Wakili wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Honestus Michael Kulaya akiwasilisha mada katika semina iliyoandaliwa na taasisi ya Landesa.

Wakili wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Honestus Michael Kulaya (mbele) akiwasilisha mada katika semina iliyoandaliwa na taasisi ya Landesa.

Wakili wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Honestus Michael Kulaya (mbele) akiwasilisha mada katika semina iliyoandaliwa na taasisi ya Landesa.

Mwakilishi wa taasisi ya Landesa na ActionAid akizungumza kufungua semina ya wadau mbalimbali kutoka asasi na mashirika ya kutetea jamii kwa ajili ya kujadili malengo mapya ya milenia 'Post 2015 Sustainable Development Agenda'.

Mwakilishi wa taasisi ya Landesa na ActionAid akizungumza kufungua semina ya wadau mbalimbali kutoka asasi na mashirika ya kutetea jamii kwa ajili ya kujadili malengo mapya ya milenia ‘Post 2015 Sustainable Development Agenda’.

Baazi ya washiriki wa semina hiyo kutoka asasi na mashirika ya kutetea jamii kwa ajili ya kujadili malengo mapya ya milenia 'Post 2015 wakifuatilia mada anuai.

Baazi ya washiriki wa semina hiyo kutoka asasi na mashirika ya kutetea jamii kwa ajili ya kujadili malengo mapya ya milenia ‘Post 2015 wakifuatilia mada anuai.

Wakili wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Honestus Michael Kulaya akijibu maswali ya washiriki semina hiyo. Kulia ni Ofisa Uchumi, Andrew Aloyce kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.

Wakili wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Honestus Michael Kulaya akijibu maswali ya washiriki semina hiyo. Kulia ni Ofisa Uchumi, Andrew Aloyce kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.

Mwakilishi kutoka UN Women, Bi. Usu Mallya akiwasilisha mada yake katika semina hiyo kwa washiriki.

Mwakilishi kutoka UN Women, Bi. Usu Mallya akiwasilisha mada yake katika semina hiyo kwa washiriki.

ACTIONAid kwa kushirikiana na taasisi ya Landesa imekutanisha wadau mbalimbali kutoka asasi na mashirika ya kutetea jamii kwa ajili ya kujadili malengo mapya ya milenia ‘Post 2015 Sustainable Development Agenda’ yanayotarajiwa kutekelezwa kwa nchi zilizokubaliana.

Akiwasilisha mada Ofisa Uchumi, Andrew Aloyce kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango alisema serikali imejipanga vema katika kutekeleza malengo mapya 17 ya Milenia yaliyopendekezwa ikiwa ni pamoja na kushirikisha asasi za kijamii na wananchi katika kuyatekeleza kila mmoja na nafasi yake.

Alisema licha ya malengo ya sasa ya milenia kuwa mengi tofauti na yaliyopita lakini utekelezaji wake kwa kila moja unategemeana huku yakiwa yamechambuliwa zaidi pamoja na kuingizwa kwenye mipango ya maendeleo katika utekelezaji wake jambo ambalo litachangia mafanikio kwenye utekelezaji wa kila lengo.

“…Malengo mapya ni mengi lakini ukisoma kwa undani kila lengo linaingiliana na lingine, hakuna linalosimama peke yake…na pia ya sasa yamechambuliwa zaidi,” alifafanua Aloyce akifafanua zaidi baada ya wanasemina kuonesha hofu ya utekelezwaji wa malengo mapya kutokana na wingi wake.

Alisema Serikali inaendelea kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili kushiriki kiufasaha katika utekelezaji wake, kwani kila mwananchi wakiwemo wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara kila mmoja ananafasi yake katika kufanikisha malengo hayo.

Aidha aliongeza licha ya kutofanikiwa vizuri kwa malengo yaliyopita lakini yapo baadhi ya maeneo nchi ilifanya vizuri sana hasa kwenye elimu na kupunguza umasikini kwa jamii. Alisema maeneo ambayo yalikuwa na changamoto kubwa ni katika malengo yaliyogusa upunguzaji vifo vya akinamama wajawazito pamoja na vifo vya watoto chini ya miaka mitano.

Kwa upande wake, Wakili wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Honestus Michael Kulaya akiwasilisha mada juu ya haki za wanawake katika suala zima la umiliki wa ardhi nchini alisema migogoro mingi ya ardhi bado inachangiwa na jamii kutokuwa na utamaduni wa kuandika usia kabla ya kifo.

Alisema suala la kujenga utamaduni wa kuandika usia ni jambo la msingi ambalo linapaswa kuzingatiwa ili kupunguza migogoro ndani ya familia, kwani kufanya hivyo mapema hakuna uhusiano na kukaribia kufa. Alibainisha kuwa watu wengi hawapendi kuandika usia mapema na wengine hudhani kuandika usia basi umekaribia kufa jambo ambalo si kweli.

Alisema kwa sasa Serikali imejitahidi kujenga usawa kati ya wanawake na wanaume katika umiliki ardhi lakini changamoto iliyopo bado akinamama wengi wanaofanikiwa kupewa ardhi wamekuwa hawaiendelezi na kungoja kuiuza hapo baadaye. Alisema taratibu zote zipo wazi na pale inapotakiwa kundi hilo kupewa ardhi hupata bila vikwazo vyovyote tofauti na ilivyokuwa huko nyuma.

Awali mwakilishi wa taasisi ya Landesa linalofanya kazi kwa ushirikiano na ActionAid alisema shirika hilo limekuwa likiwajengea uwezo jamii hasa makundi ya wanawake ili kuweza kupigania haki anuai za msingi kwao pamoja na kusaidia kutatua changamoto mbalimbali dhidi yao. Pamoja na kusaidi kampeni za usawa wa umiliki ardhi katika maeneo mbalimbali.