JARIDA la Forbes limemtaja Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kuwa mwanamke mwenye nguvu kubwa duniani. Jarida hilo limemuelezea Bi. Merkel kuwa kiongozi asiyetiliwa shaka wa Umoja wa Ulaya na ni kiongozi wa uchumi halisi duniani.
Waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Marekani, Hillary Clinton, ameorodheshwa wa pili, akifuatiwa na rais wa kwanza mwanamke wa Brazil, Dilma Rousseff, katika nafasi ya tatu. Hii ni mara ya tano kwa kansela Merkel kuongoza orodha hiyo.
-DW