Kijana Huyu Anaitaji Msaada Wako Aweze Kutibiwa…!

Kijana ABEL MACHANG'A, mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa Ukonga Mombasa Jijini Dar es Salaam, ambae anasumbuliwa na maradhi ya macho, akiwa amejipumzisha nyumbani kwao baada ya kuzungumza na waandishi wa habari ili kuomba msaada wa kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Kijana ABEL MACHANG’A, mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa Ukonga Mombasa Jijini Dar es Salaam, ambae anasumbuliwa na maradhi ya macho, akiwa amejipumzisha nyumbani kwao baada ya kuzungumza na waandishi wa habari ili kuomba msaada wa kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Kijana ABEL MACHANG’A, mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa Ukonga Mombasa Jijini Dar es Salaam, ambae anasumbuliwa na maradhi ya macho, akizungumza na waandishi wa habari ili kuomba msaada wa kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
 
 
Na Mwandishi Wetu
 
Kijana Abel mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa Ukonga
Mombasa jijini Dar es Salaam anakabiliwa na maradhi ya macho na mishipa ya
fahamu hali iliyosababisha apoteze uwezo wa kuona, na hivyo kuhitaji msaada wa
wasamaria wema ili apelekwe nchini India kwa matibabu zaidi.
Ama kweli kabla hujafa hujaumbika! Kijana ABEL MACHANG’A aliyezaliwa
miaka 23 iliyopita alikuwa na uwezo wa kuona kama kawaida na alisoma mpaka
kidato cha nne na baadaye kujiunga na elimu ya biashara katika chuo cha
biashara cha CBE cha jijini Dar es Salaam.
Lakini hivi sasa kijana huyo haoni tena baada ya kupata
maradhi ya macho yaliyosababisha macho yake kuvimba na kutoka nje licha ya
kupatiwa matibabu.
Baba wa kijana huyo amesema jitihada za kutibiwa nchini
zimeonekana kutokuwa na mafanikio na kuomba wasamaria wema na mashirika
mbalimbali yajitokeze kumsaidia kijana huyu gharama za matibabu takribani
milioni Hamsini.
Kwa yeyote atakayeguswa na maradhi ya kijana huyu,
awasiliane na Chumba cha Habari Clouds Tv Mikocheni jijini Dar es Salaam au
awasiliane na baba mzazi wa kijana huyo kwa namba 0713 275740 au 0784 275740.