Hali si Shwari ndani ya Chama cha Wananchi, CUF Dar

Baadhi ya wanachama wa CUF wakiwa wamekusanyika nje ya ofisi kuu za chama hicho Dar es Salaam wakiimba nyimbo za kumsifia Mwenyekiti wao Prof. Ibrahim Lipumba.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Magdalena Sakaya (katikati) akizungumza na wanahabari kuahirisha mkutano.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Magdalena Sakaya (katikati) akizungumza na wanahabari kuahirisha mkutano.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KUNA dalilizote kuwa hali ndani ya Chama cha Wananchi, CUF si swari ikiwa ni siku moja tu baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Seif Shariff Hamad kujitokeza katika Mkutano Mkuu wa CHADEMA na kukanusha tetesi za kujiuzulu kwa Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba.

Idadi kubwa ya wanachama wa CUF leo asubuhi wamevamia Makao Makuu ya ofisi za CUF jijini Dar es Salaam huku wakiimba nyimbo za kumsifia Mwenyekiti wao Prof. Lipumba nje ya ofisi yake na kundi la wazee wawakilishi wa wanachama hao wakidaiwa kuingia katika ofisi ya mwenyekiti huyo kwa mazungumzo zaidi.

Prof. Lupumba leo alikuwa na mkutano na waandishi wa habari majira ya saa nne asubuhi mkutano ambao ulishindwa kufanyika kutokana na wawakilishi wa wanachama hao kuwa na majadiliano ya muda mrefu na mwenyekiti hivyo kushindwa kuzungumza ya moyoni kwa waandishi wa habari.

Baada ya waandishi wa habari kukaa kwa muda mrefu wakimsubiri Prof. Lipumba azungumze kama alivyo kuwa ameto tangazo awali alijitokeza Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Magdalena Sakaya na kuzungumza na waandishi wa habari kuwa kikao cha mwenyekiti wake na wanahabari kimeahirishwa baada ya kuvamiwa na wanachama na wazee wa chama hicho leo kwa mazungumzo.

“…Nimekuja kuwajulisha kuwa Mwenyekiti aliwaita aje azungumze na nyinyi kwa jamba ambalo hata sisi hatulijui lakini asubuhi amevamiwa na wanachama ofisini kwake hadi muda huu bado yupo kwenye mazungumzo na wawakilishi wao ofisini kwake sasa nimeagizwa kuja kuwajulisha kuwa amehairisha kikao hadi hapo mtakapo julishwa tena,” alisema Sakaya.

Hata hivyo mwandishi wa habari hizi alisikia minong’ono ya baadhi ya wanachama waliokuwa nje ya jengo hilo wakilalama kuwa hawakubali kurugenzi ya chama kuendeshwa kwa kutegemea uchawi hivyo walikuwa wakitaka kujibiwa na uongozi. “…Hatukubali ulisha wahi kuona wapi kurugenzi ya chama inaendeshwa kwa kutegemea uchawi, hii haiwezekani,” alisikika mmoja wa wanachama waliokuwa wamekusanyana nje ya ofisi hizo huku wakiimba nyimbo za kumsifu Prof. Lipumba.

Taarifa ambazo hata hizo hazikusibitishwa zilidai kuwa kulikuwa na uwezekano wa Prof, Lipumba kutaka kujiusulu nafasi yake kana kwamba kuna mambo ambayo hakubaliani nayo ndani ya chama jambo ambalo wanachama walikuwa wakimzuia kuzungumza na vyombo vya habari huku wakitaka wazungumze naye kwanza ndipo aende kwa wanahabari.

Juhudu za kuwapata wasemaji wa chama juu ya taarifa zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa huwenda mwenyekiti alitaka kujiuzulu zilishindikana. Tunaendelea kufuatilia taarifa hizo na mara zitakapo tufikia tutawajuza zaidi.