Afisa Habari kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ally Changwila (kulia) akitoa maelezo kwa mmoja wa wageni waliotembelea banda la mamlaka hiyo. Afisa huyo alifafanua kuwa jukumu la kudhibiti masuala ya ki-usalama katika sekta ya usafiri wa anga nchini lipo chini ya mamlaka hiyo kwa sheria ya usafiri wa anga ya mwaka 2006 ambapo amewahamasisha Watanzania kutumia usafiri wa anga maana unatumia muda mfupi na ni wa haraka kufika eneo analokwenda abiria.
Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Masasi (kushoto) akimsikiliza Mhasibu kutoka Idara ya Pensheni Wizara ya Fedha Imelda Mzatulla (katikati) wakati wa Manesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi ambayo yanaongozwa na kauli mbiu “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”. Wa kwanza kulia ni Mchumi kutoka Idara ya Bajeti ya Serikali Wizara ya Fedha Prosper Fivawo.
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lindi na Kilwa Mwal. Mariam R. Mtima (kushoto) akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu (UTTPID) Mary Minja (kulia) leo katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.
Afisa Masoko kutoka taasisi ya UTT AMIS Waziri Ramadhani (wa kwanza kulia) akitoa maelezo ya huduma zinazotolewa na taasisi yake kwa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lindi na Kilwa Mwal. Mariam R. Mtima (kushoto) leo wakati wa Manesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.
Kikundi cha sanaa cha Mundu Arts Group kutoka Manispaa ya Mtwara Mikindani wakionesha mchezo wa sarakasi kwa wananchi waliofika kujionea masuala mbalimbali leo wakati wa Manesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.
Kikundi cha sanaa cha Mundu Arts Group kutoka Manispaa ya Mtwara Mikindani wakionesha mchezo wa sarakasi kwa wananchi waliofika kujionea masuala mbalimbali leo wakati wa Manesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.
Baadhi ya akina mama wakishiriki kazi za mikono katika shughuli za kukamilisha ujenzi wa mabanda yanayotumika wakati wa Manesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi. (Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Lindi)