Paisha Yazinduliwa Dar es Salaam…!

Mgeni rasmi ambae pia ni rais wa Makampuni ya Convivium Africa Investment, Ndg Alfonso ippolito akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa platform mpya ya matangazo iliyozinduliwa hapo jana katika hoteli ya serena.Paisha ni platform ya matangazo ambayo inapatikana kupitia simu za mkononi yaani smartphone na kupitia tovuti ambapo watumiaji wa simu za smartphone wanaweza kuipakua kupitia google play and playstore bure kabisa.

Mgeni rasmi ambae pia ni rais wa Makampuni ya Convivium Africa Investment, Alfonso ippolito akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa platform mpya ya matangazo iliyozinduliwa hapo jana katika hoteli ya serena.Paisha ni platform ya matangazo ambayo inapatikana kupitia simu za mkononi yaani smartphone na kupitia tovuti ambapo watumiaji wa simu za smartphone wanaweza kuipakua kupitia google play and playstore bure kabisa.

Meneja bidhaa wa Paisha, Godfrey Fataki akizungumzia jinsi paisha inavyofanya kazi na faida zake wakati wa uzinduzi wa platform hiyo uliofanyika jana katika hoteli ya serena

 Mgeni rasmi akifungua pazia kuashiria kuwa Paisha imezinduliwa rasmi 
Mtangazaji wa Redio Clouds Ephraim Kibonde akiwa katika picha ya Pamoja na Balozi wa Paisha wakati wa uzinduzi wa platform mpya ya matangazo iliyozinduliwa jana katika ukumbi wa Marquee Serena Hotel.
 
tukipata selfie
 Wadau wakifuatilia uzinduzi wa application ya Paisha

Paisha ni platform ambayo inapatika katika simu za smartphone pamoja na tovuti platform hii ni kwaajili ya watoa huduma na wauzaji wa bidhaa ambao wanapenda kuwafikia wateja wao kirahisi,Paisha inapatikana kupitia google play na playstore huku watumiaji wa paisha wananufaika kufahamu sehemu ambapo wanaweza kupata huduma mbalimbali kama vile maduka na hata huduma nyingine sehemu ambapo watuamiaji hao sio wenyeji au wenyeji lakini hawafahamu baadhi ya bidhaa zinapatikana wapi.

Ukiwa na application ya paisha katika simu inakusaidi kufahamu kuanzia ramani alipo mtoa huduma huyo pamoja na mawasiliano yake mfano umeenda tegeta na umepata pancha na haufahamu sehemu ilipo gereji ukiwa na paisha kwenye simu yako itakusaidia kufahamu ilipo gereji ambapo itakuonyesha jina la gereji iliyopo karibu na wewe hapo huku ikikuonyesha na ramani pamoja na mawasiliano ya gereji hiyo vilevile kwa bidhaa na huduma nyingine.

Ni application ambayo inawalete urahisi watumiaji na watangazaji wa bidhaa hizo kupitia paisha.kufahamu zaidi kuhusu paisha unachotakiwa kufanya ni tembelea tovuti yao ya www.paisha.co.tz na vilevile unaweza kupakua application hiyo kupitia playstore na google play sasa
Kuweza kupata faida zaidi