Mbwa Mwitu Waibuka Tena, Wavamia Wakata Mapanga Watu Mchana

Mtaa uliovamiwa na vibaka hao hatari wa kutumia silaha za jadi, pichani ni baadhi ya askari wakipata maelezo kwa mashuhuda waliokuwa eneo hilo wakati kundi hilo la vijana lililovamia.

Na Mwandishi Wetu,

KUNDI la vijana waporaji wanaotumia silaa za jadi baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam leo wameibuka tena na kuvamia baadhi ya maeneo ya Kigogo Luhanga, jirani na Kanisa Katoliki Parokia ya Luhanga (eneo la Jaba) na kukata watu mapanga na kupora fedha na simu.

Kwa mujibu wa mashuhuda kundi hilo liliibuka jirani na kituo cha kujiandikishia wapiga kura eneo la Jaba huku vijana wakiwa na mapanga, visu na nondo na silaha zingine zajadi ambapo waliwavamia watu na kusababisha patashika eneo hilo.

Mashuhuda wanasema baada ya kumvamia mtu mmoja jirani na grosari moja ya vinywaji vikali walimkata mapanga kichwani na kumpora fedha pamoja na simu na kumvamia mtu mwingine kisha kuanza kumshambulia jambo ambalo liliwafanya wananchi waliokuwa wakijiandikisha eneo hilo kutimua mbio huku wakiomba msaada. Baada ya tukio hilo vijana hao walianza kutishia watu na mapanga huku wakiyagonga chini kana kwamba wanayanoa kisha kutokomea mitaani.

Thehari.com ilifika eneo la tukio na kukuta tayari askari wa Jeshi la Polisi wamefika eneo hilo wakiwa na silaha kudhibiti hali hiyo, huku wakichukua taarifa kwa baadhi ya wananchi na kumkamata mmoja wa vijana ambao inadaiwa alikuwa pamoja na waporaji hao hatari. Hata hivyo askari hao hawakuwa tayari kueleza chochote juu ya tukio hilo. Mtandao huu unaendelea kufuatilia taarifa hii na kuwajuza kwa kina.