Mbeya City FC Yamsaka Muuzaji, Muagizaji Vifaa

Mbeya City FC

Mbeya City FC


Na Mwandishi Wetu,

TIMU ya Mpira wa Miguu ya Mbeya City iliyopo jijini Mbeya imetangaza zabuni kumsaka kampuni ambayo itapewa tenda ya uagizaji na uuzaji wa vifaa vyake vya michezo ili kuipatia clabu hiyo mapato kutokana na bidhaa zake.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Katibu Mkuu wa Mbeya City katika vyombo vya habari; timu hiyo imetangaza kutafuta kampuni yenye uwezo wa kufanya kazi na clabu hiyo ya kuagiza vifaa mbalimbali vya club pamoja na kuuza vifaa hivyo.

Katika maelezo ya timu hiyo imesema zabuni hiyo inafuatia utekelezaji wa club kutaka kukuza mapato yake ili iweze kujijengea msingi imara wa mapato na hivyo kuiwezesha kuendesha
shughuli zake mbalimbali.

“…Mwombaji anatakiwa atimize masharti yafuatayo; awe na leseni hai ya biashara husika, awe amesajiliwa kama mlipa kodi, awasilishe maelezo ya kampuni ‘company profile’ ikieleza aina ya kampuni au biashara unayoifanya na eneo ilipo, waombaji wawe ni makampuni yaliyosajiliwa kisheria na waambatanishe vivuli vya nyaraka zinazoonyesha uhalali wa uwepo wa mwombaji,” ilieleza sehemu ya tangazo la zabuni hiyo.