Mbunge Lembeli Aihama CCM, Atangaza Kujiunga Chadema

Bw. James Lembeli

Bw. James Lembeli


ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Kahama kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), James Lembeli ametangaza rasmi kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Akitangaza uamuzi huo Lembeli amesema amefikia uamuzi huo baada ya kushauriana na mama yake mzazi na wanafamilia. Amebainisha kuwa sababu za kukihama chama hicho ni pamoja na kukelwa na vitendo vya chuki vinavyopandikizwa na viongozi wa CCM Wilaya ya Kahama.

“Nimekaa nimetafakari tumezungumza na mama yangu kwa zaidi ya saa kumi mke wangu na watoto wangu…na kwa kusikia kilio cha wananchi wa Jimbo la Zamani la Kahama, nimeamua yafuatayo kwanza natangaza kuanzia leo kujiondoa au kufuta jina langu ndani ya Chama Cha Mapinduzi, nilikipenda lakini nimelazimika kuchukua uamuzi huu mgumu najua inawauma wengi na nawakera wengi lakini nawaomba nawao waangalie hali ambayo viongozi wa Chama Cha Mapinduzi katika Wilaya ya Kahama wamepandikiza chuki kwangu sikupenda kufanya hivyo lakini nimefanya uamuzi huu mgumu…kujiondoa na kufuta uanachama wangu ndani ya Chama Cha Mapinduzi…kuanzia leo najiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema,” alisema Lembeli leo alipokuwa akitangaza kukihama chama hicho.