Waliochukua na Kurejesha Fomu Kugombea Nafasi Anuai Leo

Mgombe ubunge viti maalumu mkoa Wa  Tanga. Wanawake ni nguzo ya maendeleo.

Mgombe ubunge viti maalumu mkoa Wa Tanga.
Wanawake ni nguzo ya maendeleo.

DHAMIRA YANGU
1. Kuwaunganisha wanawake wote Wa mkoa Wa tanga
2. Kujenga jumuiya imara ya UWT
3. Kusaidia na kuboresha maisha ya wanawake Wa makundi mbalimbali
4. Kuwa mtetezi na mwakilishi Wa wanawake katika masuala ya kijamii na kiuchumi
5. Kusaidia uanzishwaji Wa miradi ya kiuchumi ili kupambana na umasikini
6. Nitakuwa mtumishi wenu na sio kiongozi. Nichague Mimi nikawatumikie kwa manufaa ya wanawake    
     Wa mkoa Wa Tanga.
Daima wanawake ni nguzo ya  jamii.
** Chagua Josephine Mgaza***

 ‘Dogo’ Ajitosa Udiwani Kupitia CHADEMA Kata ya Korongoni Moshi

Mpambanaji aliyejitambulisha kwa mwandishi wa blog hii kwa jina la Liberatus Oba Mawalla “Dogo” (pichani juu) amechukua na kurudisha fomu za kugombea udiwani kata ya Korongoni wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Amesema endapo atapata ridhaa hatapenda wamuite mheshimiwa na badala yake anataka wapiga kura wake wamuite ndugu. Angalia picha zaidi hapa chini
Dogo akiwa na wanachama hicho
Hapa ni furaha tupu.
Dogo akiwa na vijana wa chama hicho.
Akisaini wakati akichukua fomu.
Msafara huo kurudisha fomu.
Ni alama ya vidole viwili chadema .
Ni furaha tu kwa kwenda mbele.
Ni kama wanasema ushindi ni lazima.
Msafara huo wa kwenda kurudisha fomu.
Dogo akipongezwa na vijana wenzake.

              Jerry William Silaa wa CCM Akirejesha Fomu Kuomba Ubunge

IMG_9354

Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akionyesha fomu aliyojaza kwa ajili ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 Mwaka huu nchini kote, wakati aliporejesha fomu hiyo katika ofisi za CCM wilaya ya Ilala aliyoikabidhi kwa Katibu Msaidizi wa CCM wilaya ya ILALA (kushoto). Jerry Slaa aliongozana na Mwenyekiti wa tawi la Gulukakwalala ambako ndio nyumbani kwake, Mwenyekiti wa CCM kata ya Gongo la Mboto pamoja na wazee wa jimbo la Ukonga.

IMG_9341

Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kurejesha fomu yake ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 Mwaka huu nchini kote.

IMG_9348

IMG_9317

Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi na wazee wa Ukonga aliombatana nao wakati wa kurejesha fomu.