JESHI la polisi nchini Tanzania leo limetangaza kupata mafanikio makubwa katika operation maalum inayoendelea ya kuwasaka watu waliohusika katika shambulio la kuvamia kituo cha polisi cha stakshari jijini Dar es Salaam na kuendesha mauaji ya askari wanne wa kituo hicho pamoja na raia waliokua katika kituo hicho huku wakipora kiasi kun]kubwa cha silaha na kutokomea kusikojulikana.
Akizungumza na wanahabari muda huu jijini Dar es Salaam Kamishna wa Polisi wa Kanda maalum ya Dar es salaam Suleman Kova alisema kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi wema wamefanikiwa kukamata bunduki 16 huku 14 zikiwa ni zile zilizoibiwa katika tukio la kituo cha staki shari na mbili zikiwa bado hazijulikani ziliporwa kwa watu gani.
Alisema kuwa zoezi la kuwasaka watuhumiwa hao lilianza mara baada ya kutokea kwa tukio la stakishari ambapo ilipofika tarehe 17 mwezi huu majambazi hao walijipanga kufanya tukio myinginme maeneo ya mbagala jijini Dar es salaam ambapo wananchi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na wakajipanga tayari kuwakabili.
Alisema kuwa baada ya kufika eneo la Twangoma mbagala polisi walijipanga kuwakabili na baadae majambazi hao walitokea na kuanza kushambuliana na askari hao ambapo katika mapamano hayo majambazi watano walikamatwa ambapo watatu kati yao walikuwa tayari wameshakufa na wawili wapo hai hadi leo.
Katika taarifa nyingine ambazo jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam walizipata tarehe 19 ni kuwa kulikuwa na taarifa kutoka kwa wananchi kuwa kuna tetesi kuwa silaha zilizoibiwa kituo cha stakishari zilikuwa zimefichwa katika maeneo ya mkuranga.
Jeshi la polisi liliweka kambi katika maeneo hayo na kuanza msako maalum wa kuzisaka mahali ambapo silaha hizo zilikuwa zimefichwa ambapo katika tukio la kushangaza lilionekana eneo ambalo lilikuwa limewekwa kinyesi cha binadamu na polisi kupatilia mashaka na ndipo walipoamua kupachimba na kufanikiwa kupata silaha hizo.
Baada ya kuchimba maeneo hayo jeshi la polisi lilifanikiwa kukuta silaha ambazo ni bunduku 16 ambazo 14 kati ya hizo zilitambulika ni za stakishari, na risasi 55 huku risasi 28 ni zile zilizoibiwa katika tukio la stakishari.
Pamoja na silaha hizo jeshi hilo lilikuta sanduku kubwa lililokuwa na hela kiasi cha shilingi milioni mia moja na sabini (Mil. 170) ambazo hazikujulikana mara moja zilikuwa na lengo gani huku Kamanda Kova akisema kuwa uchunguzi zaidi unaendelea.
Aidha Kamishna kova alisema kuwa pamoja na mafanikio hayo yaliyopatikana katika operation hiyo bado jeshi la polisi Kanda maalum ya Dar es salaam linaendelea na kazi kubwa ya kuwasaka wahalifu hao kwa kuwa bado kuna silaha nyingi ambazo ziliporwa katika tukio la stakishari na hazijapatikana.
Alisema katika uchunguzi walioufanya na mahojiano na baadhi ya watuhumiwa walio chini ya ulinzi Jeshi la Polisi linawatafuta watuhumiwa wafuatao; ABDULAZIZI AHMAD, ABDUL RASHID a.k.a USTAADH, ABDUL AZIZ anaishi Dar es Salaam – Kiongozi wa Kundi, SHABAN MOHAMED MTUMBUKA a.k.a AMIR SHABAN NDOBE, HANNAFI JUMANNE KAPELA MKAMBA a.k.a SHEIKH HANNAFI HASSAN HARUNA ISSA a.k.a DR. SHUJAA, ZAHAQ RASHID NGAI a.k.a MTU MZIMA, ABUBAKAR NGINDO a.k.a ABU MUHAMMAD, KHAMIS RAMADHAN, USTAADH RASHID (ambaye aliuwawa katika tukio la Sitakishari).