Wajue Walioomba Kugombea Ubunge Sehemu Mbalimbali Leo

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Octavian akimtambulisha mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini, Davis Mosha kwa wakazi wa Moshi waliofika katika uwanja wa Mashujaa.

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Octavian akimtambulisha mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini, Davis Mosha kwa wakazi wa Moshi waliofika katika uwanja wa Mashujaa.

Baadhi ya wakazi wa mji wa Moshi mjini wakiwa katika uwanja wa Mashujaa katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mtangaza nia wa nafasi ya Ubunge wa jimbo la Moshi mjini ,Davis Mosha.
Mtangaza nia ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Davis Mosha ,akiwa na meneja kampeni wake Voctor (kushoto kwake pamoja na Goodluck Moshi.
Baadhi ya makada waliofika katika uwanja huo.
Msanii wa filamu Tanzania Stephen Mengere maarufu kama Steve Nyerere alikuwa ni mmoja wa makada wa chama hicho waliofika kutoa hamasa katika mkutano  huo uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa.
Baadhi ya kina mama waliofika katika mkutano huo.
Baadhi ya vijana wakiwa na mabango yao waliofika katika mkutano huo.
Baadhi ya wananchi wa Moshi mjini waliofika katika mkutano huo wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali.
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Davis Mosha akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi.
Baadhi ya wananchi waliofika katika mkutano huo.
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Davis Mosha akisalimiana na wakazi wa Moshi waliofika katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa.
Davis Mosha akizungumza na waandishi wa habari marabaada ya mkutano wake wa kutangaza nia.
Na Dixon Busagaga

Kada wa Chama cha Mapinduzi CCM na Mwanasheria wa siku nyingi, Emmanuel Tamila Makene (kulia) akipokea fomu za kugombea kuteuliwa kugombea kuteuliwa kuwania Ubunge Jimbo la Kinondoni katika uchaguzi Mkuu utakao fanyika Oktoba 25 Mwakahuu nchini kote. Makene ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Kinondoni amechukua fomu hiyo leo, Ofisi za Chama Kinondoni Mkwajuni Dar es Salaam.

Makene akisaini kitabu kabla ya kuchukua fomu hiyo leo katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni.

 

 Makene akisikiliza maelezo kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni juu ya kanuni za kufuata kama muonesha nia.

 

Makene akionesha fomu ya kuwania nafasi ya kuteuliwa kugombea Ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM. 
 Mgombea Ubunge Jimbo la Bagamoyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mathew Juma Salum Yungwe, akionesha fomu ya kugombea nafasi hiyo baada ya kukabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, Kombo Kamote wilayani humo leo mchana.

Katibu Msaidizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Bagamoyo, Salum Mtelela (kulia), akimkabidhi stakabadhi ya malipo ya kuchukua fomu, Mgombea huyo.

 Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, Kombo Kamote (kushoto), akimkabidhi fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Bagamoyo, Mathew Juma Salum Yungwe wilayani humo leo mchana. Wa pili kulia ni Mama mzazi wa mgombea, Mary Yungwe na Meneja wa Kampeni wa mgombea huyo, James Mbuligwe.
 Hapa mgombea huyo Mathew Yungwe, akionesha fomu hiyo baada ya kukabidhiwa.
 Makada wa CCM wakimpongeza Mgombea huyo wakati wa kuchukua fomu hiyo.
 Mgombea nafasi hiyo ya Ubungo Jimbo la Bagamoyo, Mathew Yungwe (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na mama yake Mary Yungwe (kulia) na Meneja wa Kampeni wake, James Mbuligwe. Picha na Dotto Mwaibale.