Mbunge Joshua Nassar Aanguka na Helkopita…!

Helkopita hiyo ikiwa imeanguka na kukwama juu ya miti.

Helkopita hiyo ikiwa imeanguka na kukwama juu ya miti.


MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amepata ajali baada ya helkopita aliyokuwa akisafiria kupotea mawinguni kabla ya kuanguka na kukwama juu ya miti. Taarifa zilizotufikia zinasema mbunge huyo pamoja na rubani wa helkopita wamekimbizwa kwenye hospitali ya Selian Arusha kwa matibabu zaidi. Mtandao huu utakuletea taarifa zaidi za ajali hiyo baadaye.