Kinondoni Kujenga Kiwanda cha Taka…!

Taka zikiwa zimekusanywa eneo la Kinondoni.

Taka zikiwa zimekusanywa eneo la Kinondoni.


MANISPAA ya Kinondoni imesaini mkataba wa kiushirikiano na Jiji la Humburg mkataba utakaowezesha kujengwa kwa mtambo wa kuchakata taka za ugani na kuzalishwa mbolea eneo la Mabwepande wenye thamani ya shilingi za Kitanzania bilioni 3.5 fedha ambazo zote zitatolewa na jiji la Humburg.

Mkataba huo ambao utapunguza kiasi kikubwa kero ya taka katika manispaa ya Kinondoni umesainiwa leo na Mstahiki Meya pamoja na Mkurugenzi Mussa Natty. Akizungumza Mstahiki Meya alisema mtambo huu ukisha kamilika jiji la Kinondoni litakuwa safi huku likitengeneza nafasi za ajira takribani 1000 pamoja na kunufaika na mbolea kwa faida ya kilimo.