Tovuti mahiri ya habari ya modewjiblog leo imevuta umati wa watu wanaotembelea maonyesho ya 39 ya kimataifa ya kibiashara Sabasaba katika banda lake lililopo MeTL Pavillion.
Wengi kati ya watu hao walikusanyika kutaka kujua ni jinsi gani tovuti inavyofanyakazi kwa haraka na usahihi sambamba na picha za matukio yanayokuwa yamejiri kwenye habari husika.
Akitoa maelezo kwa kina Meneja mwendeshaji wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Bw. Zainul Mzige amesema ni kutokana na uelewa wa watendaji wa tovuti hiyo na kujituma kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na wananchi wote kwa ujumla.
Akitoa maoni yake wakati alipotembelea banda la Modewjiblog, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema amesema anafurahishwa sana na habari zinazoandikwa na tovuti hiyo na kuwa yeye ni mdau mkubwa kwani kila siku lazima aitembelee ili kujua dunia inaendaje.
Aidha tovuti hiyo imewataka watu wafike katika maonyesho hayo kutembelea katika banda lake ili kupata ufafanuzi wa mambo mbalimbali wanayotaka kujua kuhusu Modewjiblog na pia kutoa maoni yao.
Mrembo wa Modewjiblog, Josephine Emilian, akisimamia zoezi la wadau kutia saini kwenye kitabu cha wageni.
Mrembo wa Modewjiblog, Josephine Emilian akitoa kipeperushi kwa wadau waliotembelea banda letu.
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akitia saini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Modewjiblog katika maonyesho ya sabasaba. Kwa matukio zaidi ya picha bofya link hii