Banda la Maonyesho la Shirka la Nyumba la Taifa (NHC) lililopo langoni kuu la kuingilia kushoto kama unaingia Viwanja vya Mwalimu Nyerere kwenye Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 39 yanayoendelea.
Meneja Miradi Msaidizi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Hassan Mohammed akitoa maelekezo kwa mteja kuhusiana na namna matofali ya Hydraform yanavyotumika kujenga nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa kwenye Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 39 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba.
Afisa Mwandamizi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Salvatory Hinju akitoa maelezo namna Shirika la Nyumba linavyofanya kazi zake kwa Wateja waliofika kwenye banda la maonyesho la Shirika hilo lililopo ndani ya viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba (Mwalimu Nyerere) katika maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa
Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda akiingia kwenye viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 39 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba
Mkuu wa Ukuzaji Biashara na Masoko wa Idara ya Masoko na Mauzo ya Wizara hiyo, Zanele Sani (mwenye miwani) na Ujumbe kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara ya Afrika Kusini, wakizungumza na maafisa wa Shirika la Nyumba la Taifa kuhusu shughuli mbalimbali za Shirika.