Mabibo Beer Yadai Tirioni Moja Tume ya Ushindani

Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, James Rugemalira akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu kupinga uamuzi wa tume ya ushindani (FCC)  na kuidai fidia hiyo ya sh. tirioni moja kutoka na hasara wanayoipata kwa kuruhusu bia ya Windhoek kuingia katika soko la Tanzania ki holela.

Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, James Rugemalira akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu kupinga uamuzi wa tume ya ushindani (FCC) na kuidai fidia hiyo ya sh. tirioni moja kutoka na hasara wanayoipata kwa kuruhusu bia ya Windhoek kuingia katika soko la Tanzania ki holela.

 Mwenyekiti wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Benedicta James Rugemalira (katikati), akizungumza katika mkutano huo na kusema bia halali iliyopo kwenye soko ni ile yenye namba MB 66 na inayosambazwa na kampuni hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Mabibo, Anic Kashasha na Wakili, Stephano Kamala.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Kampuni ya Mabibo, Anic Kashasha (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Wakili wa Kampuni hiyo, Respicious Didace na Mwenyekiti wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Benedicta James Rugemalira.
 Wakili, Stephano Kamala (kulia), akizungumza katika 
mkutano huo.
 Meza Kuu. Kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Mabibo, 
Alice Marco.
 Maofisa wa Kampuni ya Mabibo wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 
Na Dotto Mwaibale
 
KAMPUNI ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd ambayo ni wasambazaji wa bia ya Windhoek inaidai Tume ya Ushindani (FCC), sh.tirioni 1 kwa kukiuka uhalali wa mkataba wa Mabibo na kudai unapingana na ushindani.
 
Katika hatua nyingine kampuni hiyo imeiomba Mahakama ya Rufaa kutoa uamuzi kuhusu uhalali wa uamuzi uliochukuliwa na Baraza la Ushindani (FCT) mwezi Aprili 2015 kuhusu haki ya Mabibo ya kuagiza na kusambaza bia za Windhoek kipekee katika soko la Tanzania.
 
Hayo yalibainishwa na Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, James Rugemalira wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana.
 
Alisema mwezi Aprili 2015, FCT ilitoa uamuzi ambao ni sawa na kutangaza kuwa mkataba kati ya Mabibo Beer Wines and Spirits na Namibia Breweries Limited uliosajiriwa kwa matakwa ya Sheria ya Alama za Biashara na Huduma wa kipee wa Mabibo haukuwa halali kisheria.
 
“Si FCC wala FCT yenye mamlaka yakutengua uamuzi halali wa Mahakama kutafsiri sheria na katiba ya Tanzania. Katika kufungua shauri lake katika Mahakama ya Rufaa tarehe 24 Juni 2015, Mabibo imeiomba Mahakama kuthibitisha kwamba mwenendo wa Mabibo ni sahihi kwa mujibu wa Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003, kama Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ilivyoamua mwaka 2010 na kuwa FCC na FCT walifanya kinyume cha mamlaka zao za kisheria na kikatiba na kujipa uwezo wa kutengua maamuzi ya Mahakama za Tanzania” alisema Rugemalira.
 
Aliongeza kuwa mbali na kuzidisha na kupanua mamlaka yao maamuzi ya FCC na FCT pia yanapuuza ukweli wa msingi. Wakati Windhoek ni bidhaa maalumu inayofahamika kimataifa, ambapo mauzo yake nchini ni kiasi cha asilimia 0.05 tu ya soko la jumla nchini na sio kampuni inayotawala soko la  bia Tanzania.
 
Alisema Mabibo inataka fidia hiyo kutoka FCC na washirika wake kwa sababu amri isiyo halali ya FCC imeruhusu muendelezo wa uagizaji wa bia ya Windhoek na wasambazaji wasioruhusiwa hivyo kuharibu biashara ya Mabibo na mkondo wa uadilifu wa bidhaa ya Windhoek katika soko la bia Tanzania.