Mwakilishi kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Vizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Mushi (wa kwanza kulia) aliyemwakilishi Dk Donan Mmbando akizungumza na washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania. Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam kwa siku mbili mfululizo.
Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dk. Jama Gulaid, akizungumza na washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania. Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam kwa siku mbili mfululizo.
Ofisa Mwakilishi Makao Makuu ya Haki za Binadamu duniani, Dk. Jyoti Sanghera.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania. Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam kwa siku mbili mfululizo.

Ofisa Mwakilishi Kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini akizungumza na washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania. Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam kwa siku mbili mfululizo.
Ofisa Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni nchini (WHO), Dk. Rufaro Chatora akizungumza na washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania. Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam kwa siku mbili mfululizo.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania. Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam kwa siku mbili mfululizo.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania. Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam kwa siku mbili mfululizo.
Ofisa mwakilishi kutoka Umoja wa Mataifa (UN), Dainius Puras akizungumza kwenye mkutano huo.
Mmoja wa waratibu wa mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania akitoa mwongozo wa majadiliano.
Ofisa Habari wa Kituo cha Taarifa cha Umoja wa Mataifa (UN), Stella Vuzo akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari vilipozungumza na viongozi wawakilishi walioshiriki katika mkutano huo.,
Ofisa Mwakilishi Makao Makuu ya Haki za Binadamu duniani, Dk. Jyoti Sanghera (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa majadiliano. Wengine ni waofisa mbalimbali walioshiriki mkutano huo wa majadiliano.
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Vizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Mushi (wa kwanza kulia) aliyemwakilishi Dk Donan Mmbando akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa majadiliano. Akiwa na Maofisa wawakilishi kutoka taasisi anuai za kimataifa zilizoshiriki majadiliano hayo.
Na Joachim Mushi, Dar es Salaam
TANZANIA inajivunia mafanikio makubwa ya kupunguza idadi ya vifo vya wajawazito pamoja na idadi ya watoto chini ya miaka mitano wanaopoteza maisha kila mwaka. Mafanikio hayo yameifanya Tanzania kutolewa mifano kimataifa ikiwa ni kati ya nchi zilizovuka malengo ya kupunguza idadi hiyo vifo iliyojiwekea kuzifikia.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Vizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando katika hotuba yake iliyosomwa na mwakilishi wake akifungua mkutano wa majadiliano na wadau mbalimbali wa utetezi wa haki za binadamu unaokutana kuangalia namna ya kupunza idadi ya vifo vinavyotokana na uzazi na vile vya watoto chini ya miaka mitano.
Majadiliano hayo yanayofanyika jijini Dar es Salaam kwa siku mbili huku yakijikita kuangalia namna wadau wa haki za binadamu wanavyoweza kuchangia katika kuboresha huduma za afya na hatimaye kumlinda mtoto chini ya miaka mitano na vifo kwa ujumla.
Dk. Mmbando alisema Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo vya uzazi na watoto, kutoka idadi ya vifo 166 vilivyokuwa vikitokea kwa kila akinamama 1,000 wanaojifungua mwaka 1990 na kupungua hadi kufikia idadi ya vifo 54 kwa kila akinamama 1,000 mwaka 2012.
Alisema mafanikio hayo ni makubwa kwani yalivuka malengo iliyokuwa imejiwekea, huku nchi ikitolewa mfano kati ya mataifa yaliyofanikiwa kiasi kikubwa kupungu vifo vya kesi za uzazi na huduma za afya kwa ujumla.
Aidha pamoja na hayo alisema bado kuna changamoto mbalimbali za upatikanaji wa huduma za afya kutoka eneo moja hadi lingine, hasa maeneo ya vijijini jambo ambalo Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inakabiliana na changamoto hizo.
Alizishukuru taasisi za Umoja wa Mataifa (UN) kwa msaada zinazoutoa kupitia taasisi zake mbalimbali kuisaidia Serikali ya Tanzania kuboresha huduma za afya katika nyanja tofauti, jambo ambalo ndio chachu ya mafanikio zaidi.
Awali akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, Mwakilishi wa UNICEF Tanzania, Dk. Jama Gulaid, aliipongeza Tanzania kwa mafanikio makubwa iliyoyapata katika kupunguza vifo vya uzazi pamoja na watoto chini ya miaka mitano na pia kuwalinda watoto katika kupata huduma bora za afya.
Aliongeza kuwa mafanikio hayo yanatokana na uongozi mzuri wa Serikali pamoja na nia thabiti ya viongozi kutambua tatizo na utayari wa kulisimamia kuhakikisha linapata ufumbuzi, lakini pia usalama wa raia na shughuli zao.
“…Napenda nitumie nafasi hii kuwasilisha shukrani na dhati kutoka UNICEF kwa Wananchi wote wa Tanzania kwa kuendelea kulinda haki za watoto, nawapongeza kinamama, nawapongeza kinababa na viongozi kwa ujumla kwa kulilinda hili…kimsingi tunaitaji mchango wenu kufanikiwa zaidi,” alisema Dk. Gulaid akiwahutubia washiriki wa mkutano huo.
Mkutano huo wa siku mbili unashirikisha wajumbe na wawakilishi kutoka taasisi za kimataifa na kitaifa zinazoshughulikia masuala ya haki za binadamu, afya na watoto umeandaliwa na Tume ya Kimataifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kushirikiana na Taasisi za Umoja wa Mataifa.