Serikali ya Watanzania Ikowapi Sabasaba..?

Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Dk. Abdalah Kigoda.

Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Dk. Abdalah Kigoda.


Mhariri pole na hongera kwa kazi nzuri ya kutupatia taarifa mbalimbali zinazo tuhusu Watanzania. Kisha napenda kutumia nafasi hii kuomba serikali ya Mh Rais Jakaya Kikwete iliyopewa dhamana na Watanzania kuwaonea huruma Watanzania kwa kuwapunguzia mzigo mzito wa malipo ya kuingia kwenye Maonesho ya Sabasaba.

Binafsi nimefika kwenye maonesho hayo lakini nilichoshuhudia jana nikwamba maonesho yamewalenga wenye kipato cha juu tu na si watanzania wakawaida asilani, kwa sababu inashangaza sana kwa serikali kuwakabidhi kampuni ya Maxmalipo kukusanya viingilio tena kwa gharama ya juu sana, Usumbufu mwingine ambao kwakweli auvumiliki, ni kwamba hawa MaxMalipo wanatoza maegesho ya magari kwa sh elfu 10, tena wanawafuata hata walio paki nje ya eneo la sabasaba, nakuwalazimisha watu walipie elfu 10 najiuliza hivi hawa wameingia mkataba wakufanya haya na nani asie na huruma na Watanzania wenye kipato cha chini?

Nimeshuhudia mzozo mkubwa pale eneo la Jeshini karibu na ATM ya NMB, mteja kaja kutoa pesa kisha wakamlazimisha alipe Tsh elfu 10 kwa kuwa ameegesha gari pale, hivi serikali kweli imejiuza kwa hawa MaxMalipo kiasi hicho?

Kwanini mliokabidhiwa mamlaka mnatufanyia hivi walalahoi? Kwanini mnatufanya tushindwe kuingia sabasaba? Mtu huyu anaenda na gari lake tena apaki viwanja vya sabasaba, mnamlazimisha kulipa eflu kumi, kisha alipie elfu 4 getini, mnatutendea haki? Isitoshe hao vijana wa MAXMALIPO wanakauli mbaya na kuonesha ubabe tena eneo la Jeshi, na nilimsikia mdada mmoja Mjeshi MP aliekuwa zamu mida ya saa nane nane mchana akimlazimisha mtu awalipe MaxMalipo Elfu 10 kwa kuwa wanahaki kulipwa tozo ya kupaki pale jeshini, hii haikukaa sawa hata kidogo.

Nashauri, Serilika ya Mkoa wa Dar es Salaam, Wizara husika, Jeshi la Wananchi na Mh. Rais na CCM chama kilicho iweka serikali madarakani kuingilia kati suala hili haraka iwezekanavyo, ili kuiepusha serikali kupata sifa mbaya mbele ya wananchi.
Haiwezekani kukawa na taratibu zisizofaa zinazo wakwaza wananchi wakipato cha chini kuingia kwenye maonesho ya SABASABA, kwanini serikali isidhibiti mapato pale mlangoni au kwenye maegesho kuliko kuingia ubia na mnadu anaeongeza garama zisizo na sababu kwa sisi walalahoi.

Nimatumaini yangu kuwa Serikali hii sikivu italiona hili na kuwashauri kwa busara walio fanya maamuzi haya ya kumkandamiza Mtanzania mwenye shahuku alieituza mwaka mzima ya kwenda Sabasaba kuachana maramoja na msimamo wao huo, maana huko ni kuendelea kuitengenezea uhasama serikali na wananchi wake hasa tunapoelekea Uchaguzi Mkuu.

Ni mimi msomaji na Mdau wa Maonesho ya Sabasaba.