Mwili wa marehemu Edson Kamukara ukiwa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Muhimbili ya Bikira Maria Salama ya Wagonjwa kwa ibada.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Muhimbili ya Bikira Maria Salama ya Wagonjwa kwa ya ibada.
Paroko wa Parokia ya Muhimbili ya Bikira Maria Salama ya Wagonjwa, Padre Ephraim Ogha akiongoza ibada ya maombi kwa marehemu Edson Kamukara.
Mwanafamilia wa marehemu Edson Kamukara akitoa salamu za shukrani kwa waombolezaji.
Mwili wa marehemu Edson Kamukara ukiwa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Muhimbili ya Bikira Maria Salama ya Wagonjwa kwa ibada.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Muhimbili ya Bikira Maria Salama ya Wagonjwa kwa ya ibada.
Mwanafamilia wa marehemu Edson Kamukara akitoa salamu za shukrani kwa waombolezaji.
Mwili wa marehemu Edson Kamukara ukitolewa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Muhimbili ya Bikira Maria Salama ya Wagonjwa baada ya ibada.
Mwili wa marehemu Edson Kamukara ukitolewa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Muhimbili ya Bikira Maria Salama ya Wagonjwa baada ya ibada.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika viwanja vya Leaders Club kutoa heshima za mwisho.
Baadhi ya waombolezaji wakishusha mwili wa Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club kutoa heshima za mwisho.
Baadhi ya waombolezaji wakishusha mwili wa Edson Kamukara katika viwanja vya Leaders Club kutoa heshima za mwisho.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa na majonzi katika viwanja vya Leaders Club kutoa heshima za mwisho.
Jeneza lenye mwili wa Edson Kamukara likiwa katika viwanja vya Leaders Club.
Baadhi ya viongozi mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP/Mwenyekiti wa Wamiliki wa vyombo vya Habari nchini, Reginard Mengi, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbroad Slaa, Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni Paul Makonda na Mbunge wa Bukoba Mjini, Bw. Kaghasheki wakiwa Viwanja vya Leaders Club kabla ya kuanza kuuaga mwili wa marehemu Kamukara.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP/Mwenyekiti wa Wamiliki wa vyombo vya Habari nchini, Reginard Mengi akisalimiana na waombolezaji wengine mara baada ya kuwasili.
Baadhi ya viongozi mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP/Mwenyekiti wa Wamiliki wa vyombo vya Habari nchini, Reginard Mengi, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbroad Slaa, Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni Paul Makonda na Mbunge wa Bukoba Mjini, Bw. Kaghasheki wakiwa Viwanja vya Leaders Club kabla ya kuanza kuuaga mwili wa marehemu Kamukara.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP/Mwenyekiti wa Wamiliki wa vyombo vya Habari nchini, Reginard Mengi akitoa pole kwa ndugu wa Edson Kamukara.
Mwakilishi wa wanafunzi waliosoma Sekondari ya Majengo na marehemu Edson Kamukara, Joachim Mushi akitoa salam za rambirambi mbele ya waombolezaji.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Kamukara.
Na Joachim Mushi, Dar es Salaam
PAROKO wa Parokia ya Muhimbili ya Bikira Maria Salama ya Wagonjwa, Padre Ephraim Ogha amewataka Watanzania na hasa waumini wa Kanisa Katoliki kujiweka tayari wakati wowote na kifo kwani kila mmoja atafikwa na tukio hilo kwa wakati wake.
Paroko Ogha alitoa tahadhari hiyo alipokuwa akihubiri katika ibada maalumu ya kumuombea aliyekuwa mwandishi wa habari na mhariri wa gazeti tando la Mwana Halisi Online, Edson Kamukara aliyefariki dunia ghafla Juni 25, 2015 nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es Salaam.
Aliwataka wanafamilia, ndugu na marafiki wa marehemu kutoendelea kusikitika zaidi kwa kifo hicho bali kumshukuru Mungu kwa tukio hilo na kuendelea kumuombea marehemu pamoja na kila mmoja kujiweka tayari na kifo. Alisema kwa kila anayeamini kuishi hana budi pia kujiweka tayari kwa kifo wakati wote ikiwa ni pamoja na kuishi maisha ya ibada huku ukimtegemea mwenyezi Mungu.
“…Kila mwanadamu anatakiwa kuishi huku akijua kipo kifo na kinakuja bila ya yeye kujua hivyo haina budi kujiweka tayari. Tunatakiwa wakati wowote tujiweke tayari katika kifo na taa zetu ziwe zinawaka wakati wote,” alisema Padre Ogha akihubiri.
Baada ya ibada hiyo mamia ya waombolezaji wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa, serikali, wamiliki wa vyombo anuai vya habari na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam walijitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Kamukara katika Viwanja vya Leaders Club kabla ya mwili huo kusafirishwa kuelekea mjini Bukoba kwa mazishi.
Miongoni mwa viongozi walioshiriki hafla hiyo ya kutoa heshima za mwisho ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP/Mwenyekiti wa Wamiliki wa vyombo vya Habari nchini, Reginard Mengi, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbroad Slaa, Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni Paul Makonda, Mbunge wa Bukoba Mjini, Bw. Kaghasheki, Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Nevill Meena pamoja na wanahabari nguli na viongozi wengine anuai.
Akizungumza katika salamu zake, Mwenyekiti wa CHADEMA, Mbowe aliwataka wamiliki wa vyombo vya habari kuangalia utaratibu wa kuwawekea bima ya maisha wanahabari wao ili kujenga mazingira ya wao kufanya kazi kwa kujiamini na kutoegemea upande wowote huku wakizingatia maadili ya taaluma yao.
Mwanahabari Edson Kamukara aliyezaliwa Kijiji cha Ihangiro, kilichopo Wilayani Muleba Mkoa wa Kagera Machi 27, 1980 amewahi kufanya kazi katika magazeti mbalimbali nchini yakiwemo, Jambo Leo, Majira, Tanzania Daima na mwishi kampuni ya Hali Halisi Publishers, wachapishaji wa Gazeti la Mwanahalisi na blogu ya Mwana Halisi.
Mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda mkoani Kagera tayari kwa mazishi.