MJUMBE wa chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania, Bw Saleh Abdallah akizungumzia kauli moja waliyokubaliana kama wasambazaji kuwa Kuanzia tarehe 1 Julai 2015 wao kama watayarishaji na wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania wamesitisha swala la kupeleka filamu zao bodi ya filamu kwaajili ya kukaguliwa wala kununua stika za TRA mpaka pale mamlaka husika zitakapokaa chini na kujadiliana kuhusu swala hili
Chama cha wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania leo wamekutana na waandishi wa habari kuelezea nia yao ya kusitisha kupeleka filamu zao bodi ya filamu Tanzania kwaajili ya kukaguliwa huku wakielezea sababu kuwa Bodi ya filamu imekua ikikagua filamu za Tanzania tu huku zile za nje zikiwa hazikaguliwi na kupelekea kuwaumiza wao katika soko la filamuĀ
Vilevile wamesitisha zoezi la kununua stika za TRA kutokana na sababu kuwa kazi nyingi za nje hazina stika na pia maafisa wa TRA wakipita kukagua filamu wanachukua za Tanzania tu ambazo hazina stika huku wakiziacha zile zinazotoka nje na zile zinaharamiwa huku sheria ya filamu ya mwaka 2012 ikisema kuwa filamu zote ziwe za nje au za ndani zinatakiwa kukaguliwa na kupewa daraja.
Kutokana na sababu ambazo chama cha wasambazaji wamezieleza kuwa Pamoja na kuwaandikia barua Mamalaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Filamu kuhusiana na swala hilo hawakuweza kupatiwa majibu ya barua yao na ndipo walipoamua kusitisha kununua stika na kupeleka filamu zao bodi kwaajili ya kukaguliwa mpaka watakapokaa meza moja huku wakiendelea kupeleka filamu sokoni.