MFUMO wa upasuaji wa kiroboti usiotumia kisu (Cyberknife) ni njia m’badala ya upasuaji usiokuwa na madhara kwa matibabu ya uvimbe wa saratani na usio wa saratani popote katika mwili, hii ni pamoja na kibofu, mapafu, ubongo, uti wa mgongo, ini, kongosho na figo. Matibabu yanayotoa mihimili ya kiwango cha juu ya mionzi kwa uvimbe uliokomaa- yanatoa matumaini mapya kwa wagonjwa duniani kote.
Mfumo wa upasuaji wa kiroboti unaotumia mionzi unaboresha mbinu nyingine za upasuaji kwa mionzi kwa kuondoa mahitaji ya baadhi ya vifaa vya upasuaji. Matokeo yake, upasuaji usiotumia kisu unawawezesha madaktari kufanikisha kiwango kikubwa cha usahihi pasipo kuwa na madhara na inaruhusu wagonjwa kutibiwa bila kulazwa.
Mfumo huu usiotumia kisu unaweza kuonesha eneo sahihi ulipo uvimbe kwa kutumia picha za mionzi (X-ray) zinazokuwa zimechukuliwa wakati wa kutibu saratani zinazoonesha utofauti wa muundo wa mifupa ya kichwa cha mgonjwa. Mfumo huu una rekodi imara ya ufanisi wa kliniki uliothibitika (Cyberknife) Tiba isiyotumia upasuaji katika kutibu saratani ya ubongo inahusisha timu, ambayo wataalamu kadhaa wanashiriki.
Timu hii inaweza kuhusisha:
• Mtaalamu wa upasuaji wa mfumo wa fahamu
• Mtaalamu wa tiba ya mionzi
• Mtaalamu wa madawa
• Mtaalamu wa mionzi
• Na madaktari wengine wasaidizi
Wakati wa hatua za awali za kupanga namna ya kutibu pasipo kutumia kisu, taarifa za ‘CT, MRI na PET scan’ zitachukuliwa kwenye mfumo wa mpango matibabu Maalum (Cyberknife Systems treatment). Timu ya madaktari itategemea ukubwa wa eneo muhimu litakalolengwa na mionzi na kiwango cha mionzi. Pia watatambua eneo ambalo mionzi itatakiwa kupunguzwa. Kwa kutumia taarifa hii, mfumo huu usiotumia kisu (Cyberknife) unatoa hesabu ya mionzi inayohitajika kutibu uvimbe husika. Mpango matibabu huu unanufaisha kikamilifu mfumo wa matibabu pasipo upasuaji kutumia kisu, inaruhusu matibabu salama na sahihi zaidi
Matibabu ya uvimbe katika ubongo hasa yanakamilika ndani ya siku 5. Kwa wagonjwa wengi, matibabu yasiyotumia upasuaji kwa kisu (Cyberknife) hauna maumivu kabisa.
Wakati wa matibabu, mgonjwa analala juu ya meza wakati uso wake ukiwa umekingwa kwa maski maalum. Mfumo huu wa kompyuta unaoongozwa kwa roboti utazunguka mwili wa mgonjwa katika maeneo tofauti tofauti ambako utafikisha mionzi kwenye uvimbe. Mgonjwa hatatakiwa kufanya chochote isipokuwa kutulia akiwa amelala kwa kunyooka ipasavyo
Tiba hii inapokamilika tu, wagonjwa wengi hurudi kwenye ratiba zao za kila siku haraka pasipo kuvuruga shughuli zao.
Baada ya kumaliza tiba ya mionzi, ni muhimu kwa mgonjwa kufwata ratiba na kuhudhuria kama atakavyoambiwa na mtaalamu. Ni muhimu pia kuelewa kuwa uvimbe hautapotea haraka. Kupona kunatofautiana kati ya mgonjwa na mgonjwa Uzoefu umeonesha wagonjwa wengi wanapokea vizuri tiba ya hii isiyohitaji upasuaji kutumia kisu. Kwa kufwatilia, madaktari wataangalia matokeo kwa miezi na miaka ya matibabu ya mgonjwa, mara nyingi kwa kutumia ama ‘CT scan’ na/au ‘PET-CT scans’.
Imechangiwa na:
Dkt RATHNA DEVI
MSHAURI MWANDAMIZI TIBA YA MIONZI
IDARA YA HUDUMA YA TIBA MIONZI NA,
MTAALAMU WA SARATANI KATIKA HOSPITALI YA APOLLO.