Paul Oops Kuwasaidia Wasanii wa HipHop…!

Paul Oops

Paul Oops


JINA la kisanii wananiita Paul Oops, nimefanya kazi na B Records Material Tabata Segerea na Chizn Brain. Nimewahi pia fanya ‘beats’ na baadhi ya wasanii wakubwa nchini huku moja ya ngoma ambayo imefanya vizuri ni no bifu ya marehemu Ngwea ft Tid.. na ambazo zipo kwa sasa ni pamoja na Leo ya Mwasiti ft Godzilla na No love ya MD Plant ft Mrap na Country Boy.

Lengo la kufanya beatstape kwanza ni kuwapa wasanii ambao hawajiwezi nafasi maana si kila msanii wa hiphop anamudu kiwango cha kurekodi tofauti na wanaoimba, kwani wao udhamini wao unakua mkubwa na soko lao linaeleweka. Hivyo niliamua kukaa na kwasababu naweza kutengeneza ‘beats’ 10 kwa siku kwanini basi nisiwasaidie hawa jamaa na kuwapa nguvu kuepuka utumiaji wa beats za watu wakati wanaweza kupata zao nzuri na mpya toka kwa maprodyuza wa nyumbani. Hivyo kila mwana hiphop anaweza kupakua ‘beats’ kwa link hii https://mkito.com/artist-profile/loopsonthebeats/7190 … thanks.