Al Shabaab Wauwa Wanausalama 15 Somalia

Wapiganaji wa kundi la Al Shabaab

Wapiganaji wa kundi la Al Shabaab


WANAMGAMBO wa kundi la Al Shabaab wamewaua walinda usalama 15 nchini Somalia baada ya kufanya shambulizi katika mji ulio karibu na Mji Mkuu wa Mogadishu. Maofisa wanasema kuwa wanamgambo hao wa kundi la Al Shabaab awali wanadaiwa kuwa walishambulia kizuizi cha polisi cha Afgoye ambapo waliwaua askari polisi watatu pamoja na kupora magari kadha.

Kisha baadaye wanadaiwa kuwavamia na kuwaua wanajeshi kadhaa. Al Shabaab wanasema kuwa wameongeza mashambulizi siku za hivi majuzi kwa sababu ni mwezi mtukufu wa Ramadhan.