INSIGNIA (Coral Paints) waanzilishi rangi rafiki wa mazingira nchini Tanzania Kuchagua rangi rafiki kwa mazingira wakati wa upambaji hakufanyi tu hewa ya ndani kuwa safi lakini pia hutunza mazingira. Hewa safi na nzuri ni jambo la kwanza kwa nyumba inayozingatia mazingira.
Kwa Bahati mbaya, kuna matatizo makubwa sana ya kiafya yanayoletwa na sumu zinazowekwa katika rangi kwa lengo la kuongeza ubora wa rangi hizo. Sumu hizi ni pamoja na risasi, zebaki, aseniki na Kromiam.
Utafiti wa mwaka 2002 uliofanywa na Taasisi ya Saratani ya Marekani ulibaini kuwa wanawake na wanaume wanaofanya biashara ya rangi wamekuwa katika hatari kubwa ya kupata saratani, matokeo yanayoonesha rangi zenye sumu zinaweza kuwa za hatari kwa afya zetu na mazingira. Shirika la afya duniani linasema kuwa wataalamu wa upambaji wana asilimia 40 ya hatari kupata kansa ya mapafu.
Wanasayansi kadhaa wamethibitisha kuwa vitu vya hatari kama aseniki, risasi na zebaki husababisha kutokea kwa magonjwa ya mishipa ya moyo. Aseniki pia inapelekea kulainisha mifupa, saratani zinazosababishwa na kromium na magonjwa ya kurithi, zebaki huweka sumu kwenye mfumo wa fahamu na figo na risasi husababisha matatizo ya saratani.
Kuanzia miaka ya 2010, wazalishaji rangi walilazimika kukubaliana na masharti ya kupunguza viwango vya sumu vinavyotumika katika rangi ili kuongeza ubora wake ikibidi hata kutotumia kabisa. Kampuni ya Insignia Limited, gwiji wa uzalishaji rangi nchini Tanzania imekuwa mzalishaji rangi wa kwanza kabisa kutoa rangi rafiki wa mazingira.
Tangu mwaka 2012 kiwanda kimechukua hatua muhimu Kuanzisha utoaji wa rangi rafiki kwa mazingira. Bidhaa zote za upambaji zinazozalishwa na kiwanda hicho hazina nyongeza ya risasi, zebaki, aseniki na kromiamu ambazo zimethibitishwa kuwa na madhara makubwa kwa afya na mazingira. Kwa mujibu wa Bw Kishan Debar Mkurugenzi mtendaji wa Insignia Limited (Coral Paints), Hatua hii ya kipekee iliyochukuliwa na kampuni inasukumwa kwa utambuzi wa wajibu wa kutunza mazingira na afya za Watanzania. Marekebisho yaliyofanyika katika rangi hayaathiri ubora wa rangi na bajeti ya mtumiaji.
“Ni kazi na wajibu wa kila mmoja kulinda mazingira wanayoishi na wanapofanyia kazi. Biashara yetu ni kufanya makazi na vitu kuwa vizuri na vya kudumu. Tunawezaje kuyasahau mazingira ambamo nyumba zetu zimejengwa. Tunafanya kila tuwezalo kusaidia kulinda mazingira tunayoishi kwa kuwa ni kitu tunachokithamini na kinachotuwezesha kuishi”. Alisema Bw Kishan akichangia.
“Haina maana kuwa ili kutengeneza rangi zinazoendana na mazingira tunaondoa ubora wake. Rangi tunazozalisha zinaenda na viwango vya kimataifa na kwa gharama nafuu, zinafanya kazi kwa kiwango cha juu, ni suluhisho lenye ubora na la kudumu lisilo na madhara”. “Coral paint inatoa rangi rafiki kwa mazingira pasipo kuongeza gharama zozote kwa mtumiaji”. Anasema Bw Kishan aliyeishukuru timu yake ya utafiti na maendeleo ndani ya Insignia Ltd.
Kuhusu Insignia Mwaka 1989, Tanzania ilishuhudia kuzaliwa Coral Paints, kampuni ndogo ambayo ingeweza kubadilisha uso wa sekta ya rangi nchini. Ikiendeshwa na dhamira ya kipekee na ubora, kampuni ambayo kwa sasa inajulikana kama Insignia Limited, ilikua kwa kiwango kikubwa na kuvuka mipaka. Hivi leo, Insignia imefikia moja ya malengo yake; ni moja ya kampuni kubwa nchini Tanzania inayoongoza katika utengenezaji wa rangi mbalimbali.
Uamuzi wake wa kuleta bidhaa zenye viwango vya hali ya juu nchini Tanzania umewezeshwa na ushirikiano na makampuni makubwa ya kimataifa kama Marmoran (Pty) Ltd, iliyopo Africa ya kusini, Ronseal iliyopo nchini Uingereza na Pat’s Deco ya Ufaransa. Bidhaa mbili za Coral na Galaxy, zinafafanua ubora wa kampuni ya Insignia. Chini ya majina haya, kampuni inatengeneza rangi na bidhaa nyingine nyingi.
Teknolojia ya hali ya juu ipatikanayo katika kampuni hiyo inaipatia kampuni hiyo msaada mkubwa sana katika ushindani. Rangi ya Galaxy inatengenezwa kiufundi, inatumia ujuzi, pembejeo na washauri wa kimataifa, inawapatia wateja wake teknolojia ya kisasa kwenye rangi. Rangi ya Coral paint ni bidhaa inayoongoza katika soko nchini Tanzania. Imepata kibali, na kuimarisha sifa yake kama bidhaa yenye ubora inayoedana na thamani- ya -fedha. Kiufanisi, miundombinu ya Insignia inajulikana kwa ubora wake.
Viwanda vyake vina vifaa vyenye ubora na vya kisasa vinavyotengeneza bidhaa zenye viwango vya kimataifa. Kampuni hii ina viwanda jijini Dar es Salaam, Moshi, Mwanza na Zambia pia ina Vituo vya usambazaji mkoani Moshi, Arusha, Mbeya na Mwanza mikoa mikubwa nchini. Pia kuna uwepo wa mtandao mpana wa wafanyabiashara na malori ya kisasa kuwahakikishia usambazaji wa bidhaa nchini kote. Kampuni hiyo pia ina vituo nchini Rwanda, Burundi na Malawi.