Serikali inadhamira yadhati kuboresha huduma ya ardhi nakuipeleka karibu na wananchi kwa wakati ili iwe na tija kwa maendeleo endelevu.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alipokuwa akiongea na Balozi wa Ireland nchini Tanzania Bi Fionnuala Gilsenan leo jijini Dra es salam.
Akifafanua kuhusu namna huduma hiyo itakavyopelekwa karibu na wananchi, Waziri Lukuvi amesemakuwa wizara yake imeanzisha kanda nane ili kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi badala ya hali ilivyokuwa zamani ambapo huduma hizi zilitolewa makao makuu ya wizara hiyo tu yaliyopo jijini Dar es salaam.
“Ili kutoa huduma ya ardhi kwa wakati kwa wananchi, huduma ya utoaji wa Hatimiliki za ardhi sasa ni kwenye kanda ambazo zinasimamiwa na Makamishna wa Ardhi Wasaidizi.” Alisema Lukuvi.
Kanda hizo ni kanda ya Dar es salaam inayojumuisha Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni, kanda ya Mashariki ambapo makao makuu yake yapo Morogoro, kanda ya Magharibi makao yake makuu yapo Tabora, kanda ya Ziwa makao yake makuu yapo Mwanza na kanda ya Kaskazini makao yake makuu yapo Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kanda nyingine ni pamoja na kanda ya kusini ambayo makao yake makuu yapo Mtwara, kanda ya Kusini Magharibi makao yake makuu yapo Mbeya na Kanda ya Kati ambayo makao yake makuu yapo mkoani Dodoma.
Katika kutoa huduma yenye ubora kwa wananchi kwa wakati, Serikali kwa kushirikiana na Halmashauri wataongeza watumishi wakada za wapimaardhi, wapangaji wa miji na vijiji pamoja na wathaminia mbao watafanyakazi kwa pamoja kwenye kanda husika ambapo huduma ya ardhi itakuwa karibu zaidi na wananchi.
Naye Balozi wa Ireland nchini Tanzania Bi Fionnuala Gilsenan amempongeza Waziri Lukuvi na watendaji wote wa wizara hiyo kwa kuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma haraka na kwa wepesi zaidi kwa jamii hatua ambayo ni yakupongezwa na kila mpenda maendeleo.
Balozi Bi Gilsenan alisema kuwa ardhi nibidhaa muhimu inayoweza kutumika kwa kutoa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo elimu, maji, barabara, ujenzi wa viwanda na miundo mbinu mingine ili kumfanya mwananchi kupata huduma yenye tija kwa wakati.
Aidha, kwa upande wake Kamishna wa Ardhi nchini Dkt. Moses Kusiluka alisema kuwa utoaji wa huduma ya usimamizi wa ardhi umeanza kuboreshwa kwa kubadili mfumo wa utoaji wa huduma kuwa wa kielekroniki kutoka mfumo wa kawaida, yaani‘manual’.
Dkt. Kusiluka amesisitiza kuwa mfumo wa kielektroniki utaboresha sana utoaji wa huduma za ardhi, ikiwa ni pamoja nak uondoa tatizo la milkipandikizi (double allocation), kuondoa udanganyifu, kuongeza ufanisi wa watendaji na kuongeza mapato ya Serikali.