Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake ya mwisho kwenye kikao cha Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika kinachofanyika kwenye Ukumbi wa Sandton jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini tarehe 15.6.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akijiandaa kutoa hotuba yake ya mwisho kwenye Mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika unaofanyika huko Johannesburg Afrika Kusini tarehe 15.6.2015.
Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wao wa mwaka unaozungumzia uwezeshaji kwa wanawake na Maendeleo katika Bara hili.
Mke wa Rais Mama Saloma Kikwete akiangalia moja ya machapisho mbalimbali yanayohusiana na Mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika (OAFLA) unaofanyika nchini Afrika Kusini.