Timu ya Soka ya ‘Bongo Starz’ yaendelea na mazoezi! Pt 1

Wachezaji wa Bongo Starz wakiwa wamejipanga tayari kuanza kupasha viungo moto

Na Muandishi wetu, Los Angeles

Timu ya Watanzania waishio kusini mwa California jana Jumamosi walikutana kwa mara nyingine tena, kwa ajili ya mazoezi kabla ya mechi za mataifa mbalimbali kuanza hapo September 3, 2011 na kumalizika tarehe hiyohiyo. Mashindano hayo yatafanyika jijini Los Angeles, California.  dev.kisakuzi.com, ilikuwepo uwanjani kushiriki na pia kushudia jinsi timu ilivyokuwa inafanya mazoezi ya nguvu katika upande wa pumzi na viungo, ili kujihakikishia ushindi katika mashindano hayo. 

Kapteni wa Bongo Starz, ndg. Jovis Temu alisema, “Inaonekana litakuwa shindano zuri, pia lililopangiliwa. Hamna mtu anayelipwa kushiriki katika mashindano haya, sie wote tunajitolea. Kwa hiyo naomba sana kila Mtanzania na wote wanao ipenda nchi hii waje kujumuika na kushangilia. Mshindi wa kwanza atachukua $3000, kombe moja la timu na medali kwa kila mchezaji. Hili sio kombe la Mbuzi au Ng’ombe”  alimalizia kusema.

Bongo Starz itakutana tena Jumamosi ya tarehe 27 na tarehe 28 Jumapili, kabla ya michuano kufanyika Sept 3.  Zifuatazo ni picha mbalimbali za mazoezi hayo.

Wachezaji wa Bongo Starz wanaonekana wakipasha viungo moto kabla ya kuanza kusakata kabumbu

Mchakamchaka ukiendelea

Mkurugenzi wa Bodi ya Watanzania waishio kusini mwa California, Ndg. Iddy Mtango akiwa mstari wa mbele

Washangiliaji pia walikuwepo

Mshambuliaji hatari wa Bongo Starz, Rungwe Jr. akipiga pozi na mshehereshaji, Gabriel

Wachezaji wakiwa tayari wamejigawa makundi mawili tayari kwa kuanza mchezo wa kujipima viwango

Wachezaji wakiwa wanapata mawili matatu kutoka kwa Kapten Jovis (Aliyekaa,Mwenye jezi nyekundu), baada ya mazoezi kwisha

maelezo yakiendelea

Picha zote na mpigapicha wa thehabari, Los Angeles.