Barcelona ni Nooomaa, Waiuwa Juventus Watwaa Ubingwa

Wachezaji wa Barcelona wakishangilia ubingwa

Wachezaji wa Barcelona wakishangilia ubingwa

TIMU ya Barcelona imetawazwa Mabingwa wa Ulaya kwa mara ya tano baada ya kufanikiwa kuichapa timu ya Juventus mabao matatu kwa moja (3-1) katika mechi kali ya fainali iliochezwa katika uwanja wa Olimpiki wa mjini Berlin.

Timu ya Barcelona ndiyo waliokuwa wa kwanza kufunga kupitia kwa mchezaji wake Ivan Rakitic mnamo dakika ya nne tu ya mwanzo baada ya kuanza kwa mtanange huo mkali.

Hata hivyo Alvaro Morata alifanikiwa kusawazisha goli hilo. Mchezaji Luis Suarez aliifungia tena bao jingine baada ya kipa Gianluigi Buffon kuutema mpira wa staa wa Barcelona Messy. Ikiwa kama bahati kwa Barcelona nyota wake mwingine Neymar alifunga kitabu cha mabao ya timu yake baada ya gusa ni guse kati yake na Messy.

Katika mechi hiyo Andre Iniesta ndiye aliyetangazwa mchezaji bora katika mchezo. Hii inamaanisha kwamba Barcelona wameshinda mataji matatu ikiwemo lile la Copa Del Rey, La liga na la vilabu bingwa barani Ulaya.

Mechi hiyo pia ilikuwa ya mwisho kwa kiungo wa wakati wa Barcelona Xavi Hernandez ambaye anaondoka kilabu hiyo baada ya kuichezea kwa muda mrefu.
-BBC