Balozi wa StarTimes nchini, Msanii Nurdin Bilal ‘Shetta’ (katikati), akiwa na wadau wengine kwenye uzinduzi huo.
Na Dotto Mwaibale
BALOZI wa China nchini Tanzania, Liu Dang amesema ushiriano wa kirafiki baina ya Tanzania na China ni muhimu sana katika ukuzaji wa sekta ya utamaduni.
Kauli hiyo aliitoa wakati akihutubia katika uzinduzi wa Tamthilia ya Tuonane ‘Lets Get Married iliyochezwa na wachina baada ya kutafsiriwa kwa lugha ya kiswahili.
“China na Tanzania ndugu na ushirikiano na ubadishilianaji katika sekta mbalimbali hasa sekta ya kiutamaduni zinahistoria ndefu hivyo zinapaswa kudumishwa” alisema Balozi Dong.
Alisema Rais wa China Xi Jingping alipotembelea Tanzania mwaka jana serikali za hizi nchi mbili zilipeana vizuri mawazo na kusaini mikataba mingi mbalimbali ya ushirikiano ambapo ziara hiyo iliziletea nchi hizi mbili mafanikio makubwa na kufungua ukurasa mpya wa maendeleo ya historia ya uhusiano baina yao.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mchambuzi wa Vipindi wa Kampuni ya StarTimes Tanzania, Rehema Kisyombe alisema kutokana na ushiriano mzuri wa nchi hizo kwa upande wao StarTimes wameadhimia kuudumisha kwa njia ya burudani kwa kuleta vipindi mbalimbali kutoka china.
Alisema kwa kutambua hilo StarTimes imekuwa ikileta tamthilia mbalimbali za kichina zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ambapo mpaka hizi sasa wamekwisha onesha nne kupitia chaneli ya Kiswahili ijulikanayo kwa jina la Star Swahili.
Kisyombe alizitaja tamthilia hizo kuwa ni Mapambano, Ujana wangu, Matumaini ya Baba na Hot Mom ambazo zilipokelewa vizuri na watamazaji wa chaneli hiyo na sasa wanawaletea tamthilia hiyo ya Tuoane.