Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maafikiano yaliyotokana na itifaki ya pamoja kwa nchi za SADC inayohusu udhibiti wa fedha chafu na katiba ya ushirikiano wa majeshi ya Polisi kwa nchi wanachama wa SADC yaliyoafikiwa katika mkutano wa 31 wa Viongozi wa Nchi wanachama wa SADC mjini Luanda Angola Agosti 18. (Picha na Amour Nassor-OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikaguwa gwaride lililoandaliwa maalum kwa ajili ya kumuaga wakati alipokuwa akiondoka uwanja wa ndege wa Fevereiro uliopo jijini Luanda, Angola Agosti 19, baada ya kumalizika kwa mkutano wa 31 wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika Agosti 18. (Picha na Amour Nassor-OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Mogan Tsvangirai, walipokutana kwenye mkutano wa 31 wa Viongozi wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) nchini Luanda Angola (Picha na Amour Nassor-OMR)
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe na Wajumbe kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya ya Maendeleo zilizopo Kusini mwa Afrika (SADC), wakiwa katika mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya hiyo nchini Luanda, Angola (Picha na Amour Nassor-OMR)