Walemavu Wafunga Barabara ya Kawawa Dar, Shughuli Zasimama

Baadhi ya walemavu wafanyabiashara katika soko la Mchikichini, Karume jijini Dar es Salaam wakiwa wamefunga barabara za makutano ya Kawawa na Uhuru jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya askari wa jeshi la polisi wakiwa eneo la tukio huku wakiendelea kushawishi wafanyabiashara hao waondoke barabarani ili shughuli zirejee.

Baadhi ya wananchi wakilazimika kutembea kwa miguu eneo la Karume baada ya kushuka kwenye magari yalioko kwenye foleni huku wafanyabiashara katika soko la Mchikichini, Karume jijini Dar es Salaam wakiwa wamefunga barabara za makutano ya Kawawa na Uhuru jijini Dar es Salaam.

WAFANYABIASHARA ndogondogo wenye ulemavu eneo la Mchikichini, Karume jijini Dar es Salaam wamefunga barabara kwa zaidi ya saa nne wakishinikiza kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ili wafikishe kilio chao cha kuvunjiwa maeneo yao ya Biashara pamoja na kuibiwa mali zao wakati wa zoezi la vunjavunja mabanda na meza zao za biashara.

Zoezi la uvunjaji limefanyika usiku wa kuamkia leo ambapo Manispaa ya Jiji walivamia maeneo hayo na kuvunja meza na vibanda vya wafanyabiashara hao wakiwemo watu wenye ulemavu mbalimbali. Taarifa zinasema zoezi hilo limefanywa na jiji ikiwa na oparesheni ya kuondoa wafanyabiashara wanaofanya maeneo yasio rasmi.

Baada ya walemavu kukuta meza na mabanda yao yamevunjwa asubuhi waliandama hadi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick wakitaka wazungumze naye kujua hatma ya biashara zao ambazo wanadai zimevunjwa na baadhi ya mali kupotea. Baada ya juhudi za kuonana na Mkuu wa Mkoa kugonga mwamba waliamua kulala barabarani na kuziba barabara za makutano ya Kawawa na Uhuru jambo ambalo lilileta kero kubwa kwa watumiaji wa barabara hizo.

Shughuli zililazimika kusimama hasa kwa wafanyabiashara wa usafirishaji na watu wengine kuanzia majira ya saa nne asubuhi hadi saa nane mchana kabla ya ufumbuzi kupatikana juu ya mzozo huo. Wananchi walilazimika kushuka kwenye magari na kuanza kutembea kwa miguu kuvuka eneo hilo huku kukiwa na msongamano mkubwa wa magari hata barabara nyingine za mchepuko eneo hilo.

Juhudi za Jeshi la Polisi kuwashawishi walemavu hao kutoka ziligonga mwamba na kulazimika kukaa nao eneo la tukio huku wakiendelea kuwaomba waondoke eneo hilo ili shughuli nyingine za matumizi ya barabara hizo ziendelee lakini waligoma huku wakimtaka Mkuu wa Mkoa aje eneo hilo awaeleze hatima yao na bidhaa zao.

Majira ya saa nane mchana ulipatikana ufumbuzi ambapo baadhi ya viongozi wa wafanyabiashara hao walifanya mazungumzo na uongozi wa mkoa na kukubaliana waondoke na kesho utaratibu utafanywa wa mazungumzo pamoja na tathmini kwa waliovunjiwa ili jiji liwalipe. Uongozi katika makubaliano ulikiri kuna makosa yamefanyika hivyo mazungumzo yatafanywa kwa pande zote na tathmini kabla ya fidia kuanza kulipwa. Hata hivyo katika makubaliano hayo wamekubaliana walemavu hao kuendelea kufanya biashara zao hadi pale ufumbuzi utakapo patikana.