Mbunge Mtemvu Afanya Ziara Kuangalia Miundombinu ya Majitaka

Meneja wa Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Julius Ndyamukama akiwa na (wa tatu)kulia akizungumza jambo wakati wa ziara na Mbunge Abbas Mtemvu wakati wa ziara hiyo

Meneja wa Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Julius Ndyamukama akiwa na (wa tatu)kulia akizungumza jambo wakati wa ziara na Mbunge Abbas Mtemvu wakati wa ziara hiyo

  Diwani wa Soko la Tazara Vetenary Zahoro Maganga akitoa maelezo kwa Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu alipotembelea maeneo yaliyoharibiwa  na mvua akiongozana na  viongozi wa Wakala wa Serikali wa Barabara (Tanroads) jinsi maji yanavyotakiwa kufata mfereji huo ambao haupitishi maji kupeleka katika mfereji huo .
 
 Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (kulia) akizungumza na viongozi wa Wakala wa Serikali wa Barabara (Tanroads)  katika ziara ya kutembelea maeneo yaliyo haribiwa na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam (kushoto) ni Meneja wa Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Julius Ndyamukama.
 Mhandisi Mradi Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam Ngusa Julius (wa pili kulia)  akimwelekeza jambo Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (aliye vaa kofia) wakati wa ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya jimbo lake yaliyo haribiwa na mvua na kusaidia kutowa Mashine ya kuondoa  maji hayo yaweze kuondolewa (kushoto) ni Katibu wa Kamati ya maafa na miundombinu ya Soko la Vetenary Manispaa ya Temeke  Morocco Milanzi na kulia ni Naibu Meya Manispa  Temeke Juma Mkenga
Katibu wa Kamati ya maafa na miundombinu ya Soko la Vetenary Manispaa ya Temeke  Morocco Milanzi (wapili kulia) akizungumza na viongozi wa Wakala wa Serikali wa Barabara (Tanroads) wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (wa pili kushoto), wakati wa  ziara ya kutembelea maeneo yaliyo haribiwa na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam na mbunge huyo kusaidia mashine ya kuyaondosha maji hayo
 Baadhi ya maeneo waliyo kumbwa na maji katika  Soko la Vetenary Manispaa ya Temeke. PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)