Na Anitha Jonas – MAELEZO
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe amefungua Mkutano wa Tisa wa Baraza la Wafanyakazi uliolenga kujadili masuala mbalimbali ikiwemo urejeshaji wa wafanyakazi wa wizara yake walioko nje ya nchi.
Hayo yasemwa leo na Waziri Membe alipokuwa akifungua mkutano huo ulihusisha wafanyakazi wa Wizara pamoja viongozi wa TUGHE, kwa lengo la kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha mazingira ya kazi kwa kila mtumishi wa Wizara hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
“Tunatarajia kupata bilioni 300 zitakazotusaidia kuwarudisha nchini wafanyakazi wote 45 wa Wizara waliomaliza mikataba yao kazi huko nje ndani ya miezi mitatu, ilikuwapa nafasi wafanyakazi wengine nao kwenda kutekeleza shughuli walizokuwa wakizifanya wa kwani hii inasaidia kuwapa fursa mkubwa kila mtumishi wa kupata ujuzi mkubwa kutoka kwa watu wengine,” alisema Membe.
Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Diaspora Bibi. Rose Jairo wa alimpongeza Waziri Membe kwa juhudi zake mbalimbali alizozifanya katika Wizara hiyo ikiwemo kuanzisha kitengo cha Diaspora pamoja kukisimamia kwa madhubuti katika kuhakikisha kinafanya kazi kwa uhakika na kuleta tija kwa Serikali.
“Mhe. Waziri tunakupongeza kwa jitihada zako ulizozifanya katika Wizara yetu pia umekuwa kiongozi mwenye kujali maslahi ya kila mtumishi na pia kuna mambo mengi mazuri umeyafanya ikiwemo kuboresha maslahi ya wafanyakazi kuwapa nafasi za kwenda kusoma nje na kuwatafutia nafasi za mafunzo nje,” alisema Bibi Jairo.
Mbali na hayo naye Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Gaudensi Kidingo aliipongeza wizara ya mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa kwa kuzingatia ratiba na kuweza kufanya vikao vyote vya wafanyakazi, pia ameiomba wizara kujaribu kuzingatia muda wa kufanya mkutano wa Baraza la wafanyakazi ili TUGHE wawezekupata muda mzuri wa kushauri menejimenti.