Mradi wa Maboresho Matumizi ya Fedha za Umma Wafanikiwa

Msemaji wa Wizara ya Fedha, Bi. Ingiahedi Mduma (wa kwanza kulia) akitoa ufafanuzi kwa wanahabari wanaoshiriki semina juu ya taarifa ya Mradi wa Maboresho ya Matumizi ya Fedha za Umma (PFMRP).

Msemaji wa Wizara ya Fedha, Bi. Ingiahedi Mduma (wa kwanza kulia) akitoa ufafanuzi kwa wanahabari wanaoshiriki semina juu ya taarifa ya Mradi wa Maboresho ya Matumizi ya Fedha za Umma (PFMRP).


Baadhi ya maofisa wa Wiazara ya Fedha wakiwa kwenye semina ya waandishi wa habari pamoja na waandishi wa habari katika mitandao ya jamii.

Baadhi ya maofisa wa Wiazara ya Fedha wakiwa kwenye semina ya waandishi wa habari pamoja na waandishi wa habari katika mitandao ya jamii.

Mhariri wa mtandao wa dev.kisakuzi.com ambaye pia ni Mwenyekiti wa Muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachimi Mushi (wa pili kulia) akiuliza swali katika semina hiyo.

Mhariri wa mtandao wa dev.kisakuzi.com ambaye pia ni Mwenyekiti wa Muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachimi Mushi (wa pili kulia) akiuliza swali katika semina hiyo.

Baadhi ya wanahabari wanaoshiriki Semina ya Siku tatu iliyoandaliwa na wizara ya fedha mkoani Pwani wakifuatilia semina hiyo.

Baadhi ya wanahabari wanaoshiriki Semina ya Siku tatu iliyoandaliwa na wizara ya fedha mkoani Pwani wakifuatilia semina hiyo.


Na Joachim Mushi, Kibaha

MRADI wa Maboresho ya Matumizi ya Fedha za Umma (PFMRP) umefanikiwa kuboresha nidhamu ya matumizi ya fedha za umma hasa katika eneo la ukaguzi wa fedha katika taasisi na idara mbalimbali za Serikali. Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Kibaha na Msemaji wa Wizara ya Fedha, Bi. Ingiahedi Mduma alipokuwa akifafanua taarifa ya PFMRA kwa wanahabari wanaoshiriki semina ya siku tatu iliyoandaliwa na wizara hiyo.

Akizungumzia mradi huo alisema umepata mafanikio makubwa hasa ya kuweka mfumo mzuri wa malipo, muda wa kupitishwa kwa bajeti ya Taifa umeimarika na fedha zinatoka kwa wakati. Aidha bajeti ya mwananchi inatangazwa katika Tovuti ya Wizara ya fedha. Aliongeza kuwa mtandao wa malipo umefika mpaka katika Serikali za Mitaa.

Bi. Mduma alisema PFMRP ni mradi wa maboresho ya matumizi ya fedha za umma ulioanzishwa na Serikali ya Tanzania kwa madhumuni ya kuimarisha mifumo ya matumizi ya fedha katika ngazi zote.

Alisema maboresho ya fedha za umma yanaenda sanjari na maboresho katika sekta za umma ambayo yanalenga kuimarisha utendaji bora na makini katika kutoa huduma ambazo zinaimarisha na kukuza uchumi wa taifa. Alisema mpango huo sasa imeingia awamu ya nne na unatarajia kusimamia na kuwajengea uwezo wanaofanya shughuli za maboresho ya fedha za umma katika Nyanja mbalimbali.

“…Madhumuni ya mradi huu katika awamu ya nne umelenga katika kuongeza nguvu ambayo itawezesha kufikia malengo ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025, hiyo inaenda sanjari na mpango wa maendeleo wa miaka mitano yaani 2011/2012 – 2015/2016 na MKUKUTA (Mkakati wa Kukuza uchumi Tanzania)/MKUZA (Mkakati wa Kukuza uchumi Zanzibar), ili kufika malengo ya ukuaji wa uchumi,” alisema.

Aidha alisema mafanikio ya mradi huo ni katika eneo la uimarisha matumizi mazuri ya fedha za umma yatafikiwa kwa kuwa na matokeo ya maeneo makuu matano kama vile, usimamizi wa ukusanyaji kodi, mpango wa bajeti, usimamizi wa bajeti, uwazi na uwajibikaji, simamizi wa matumizi ya fedha zilizopangwa kutumika na kugundua matumizi yanayoweza kujitokeza baadae na mabadiliko ya Uongozi pamoja na uangalizi na mawasiliano kwenye mambo yafedha.

Alibainisha kuwa mradi huo unafanya tathmini katika uwigo uliowekwa kwa kuangalia vipaumbele ambavyo vitatoa muelekeo na kufikia matokeo mazuri. Ili kuhakikisha kuwa ripoti za fedha zinazotolewa zinakuwa za aina moja bila kuwa na utofauti wa aina yoyote. Kuwa na uongozi mzuri ambao umepanga vizuri Taasisi za fedha.

Kuzilenga na kuzipa nguvu wakala ambazo zinaguswa moja kwa moja katika mifumo ya fedha za umma. Mradi huu unafadhiliwa kwa pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB na Bank ya Dunia (WB), DfID, CIDA, DENMARK, IRELAND na KFW. Hawa wote walisaini makubaliano ya kuchangia katika mradi huo.

Awamu ya kwanza ilikuwa kutoka mwaka 1998 – 2004 huu ulikuwa na malengo ya kudhibiti matumizi, kuweka nidhamu ya fedha pamoja na kukuza na kuimarisha uchumi mpana. Awamu ya pili (II) ilikuwa kutoka mwaka 2004 – 2008 malengo ya mradi huo yalikuwa ni kuimarisha na kuendeleza mifumo na njia zinazotumika katika malipo ya fedha za umma kwa kutumia njia rahisi na zana nyepesi.

Aidha awamu hiyo ilizingatia pia uimarishaji wa njia ya ukusanyaji mapato na jinsi ya kuweka mbinu ya kuzitumia rasilimali fedha na kuweka mikakati ya kipi kianze kwanza.

Awamu ya tatu (III) ilikua kuanzia 2008 – 2011, mradi huu ulikua na malengo ya kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji rasilimali fedha kutoka katika Taasisi mbalimbali za kifedha. Awamu ya nne (IV) ya mradi ni kuanzia June 2012, mradi ulizinduliwa na kuanza rasmi tarehe 1 Julai, 2012.