Meneaja wa NMB kanda ya kasakazini Vicky
Bishubo akikabidhi msaada kwa mkuu wa wilya ya Hai, Anthony Mtaka huku
zoezi hilo likishuhudiwa na mbunge wa jimbo hilo Freeman
Mbowe.
|
Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kaskazini
Vicky Bishubo akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa kwa waathirika
wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni ukanda wa chini wilayani
Hai. |
|
Msaada wa magodoro uliotolewa na Benki ya
NMB kwa waathirika wa mafuriko yaliyotkea hivi karibuni wilayani
Hai. |
|
DC Mtaka,Mbunge Mbowe na Meneaja wa NMB
,Bishubo wakifurahia msaada huo. |
|
Msaada mwingine uliotolewa ulikuwa ni wa
Blankets. |
|
Chakula pia kilitolewa kwa wahnga
hao. |
|
Meneaja wa NMB,Vicky Bishubo akiwa na
wahanga wa mafuriko .
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda
ya Kaskazini.Benki ya NMB
imetoa msaada wa kibinadamu wa vifaa mbalimbali
vyenye thamani ya zaidi ya shilingi
milioni 10 baada ya kutembelea eneo la tukio na kujionea athari kubwa zilizosababishwa na
mafuriko hayo.Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo Meneja wa
NMB kanda ya Kaskazini, Vicky
Bishubo,alitoa pole kwa familia zilizofikwa na
kadhia hiyo huku akisema NMB imeguswa
na tukio hilo na kwamba inatoa msaadakatika maeneo
matatu.
Alisema eneo la kwanza la msaada ni chakula ambapo imetoa unga
kilo 2,000,Maharage Kilo 500,Sukari
Kilo 500 na mafuta ya kula lita 1,000.Eneo jingine ni eneo la malazi ambapo yametolewa
Magondoro 70,Mablangeti
100,pamoja na marobota ya nguo huku pia Benki hiyo ikichangia mifuko 50 ya Sementi kwa ajili ya
ukarabati wa shule ya msingi
Elerai iliyofikwa pia na mafuriko.“Tumesikitishwa na
majanga yaliowakuta,NMB tumekuwa na desturi ya kurudisha faida yetu katika jamii kwa kusaidia
majanga mbalimbali hivyo tumetoa
msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingimilioni 10”alisema
BishuboNao baadhi ya wahanga wa mafuriko hayo
waliishukuru NMB kwa msaada huo na kutoa rai kwa watu,mashirika na taasisi
mbalimbali zilizo za kiserikali na
zisizo za serikali kuona umuhimu wa kuendelea kutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu kutoka na adhari
ziliwakumba.Mwisho. |