MAXCOM Maxcom Africa maarufu kama MaxMalipo ni kampuni ya kitanzania iliyoanzishwa mwaka 2010
ambayo imewekeza katika kurahisisha maisha ya Watanzania na Waafrika kwa ujumla
kiuchumi na kijamii kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano (ICT
Technology).

Ili kufikia malengo na Sera ya Taifa ya kutumia mifumo ya kielekroniki kutoa huduma
na pia kuwezesha Watanzania walio wengi kufikiwa na huduma hizi (Financial
Inclusion) na pia kurahisisha ukusanyaji wa kodi na kuongeza
ajira, MaxMalipo imeanzisha huduma mpya
itakayomuwezesha mtanzania kulipa bili zote kwa kutumia simu ya kiganjani aina ya
Smart phone yenye Mfumo utakaojulikana kama SmartMalipo.

Huduma hii inatarajiwa kutoa ajira kwa watanzania takribani laki mbili (200,000) nchi nzima kufikia mwaka 2016 na hivyo kuchangia ukuaji wa sekta isiyo rasmi
ya ajira na kunyanyua uchumi wa Nchi.
ya ajira na kunyanyua uchumi wa Nchi.
Mfumo huu utaweza kurahisisha ulipaji wa bili mbalimbali Mfano; Umeme
(Luku), Ving’amuzi vya Televisheni, Vocha za Mitandao yote, Kulipia Kodi za TRA
na Baadae Kufanya Miamala ya Kibenki inayohusisha Kuweka na Kutoa fedha, huduma
ambazo kwa sasa zinalipwa kupitia mashine za MaxMalipo.
Huduma hiyo inapatikana kwenye mfumo wa simu ya kiganjani ambapo mtumiaji atalazimika
kuweka mfumo wa SmartMalipo (Download
Smart Wakala Application) kutoka tovuti ya Google play au tovuti ya Maxmalipo
kwa kuandika neno ‘SmartMalipo au Maxmalipo’.

Kisha mtumiaji atapata maelekezo ya jinsi ya ku-install mfumo huu
kwenye simu yake na jinsi ya kutumia. Mfumo huu utamwezesha mtumiaji yeyote kuwa
Wakala na kulipia huduma zilizo orodheshwa. Mtumiaji
wa mfumo huu atajipatia kamisheni kama alivyo wakala
mwingine wa Maxmalipo kwa Huduma atakazofanya.

Watumiaji wa mfumo huu wa SmartMalipo watatambulika kwa jina la ‘Smart Wakala’ popote
walipo na kufanya biashara kupitia simu zao za kiganjani. MaxMalipo
imeanzisha huduma hii mpya kwa lengo la kuwawezesha watanzania walio wengi
kufikiwa zaidi na huduma za malipo kwa haraka wakiwemo wafanyabiashara wadogo na wenye mitaji midogo ambao kwa mazingira yao ni vigumu kuwa na
Mashine za Maxmalipo.

MaxMalipo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza matatizo ya foleni kwenye malipo ya huduma mbalimbali kama bili za TRA, LUKU, DAWASCO, huduma za kibenki na hata katika mifuko ya Hifadhi ya jamii Mfano PSPF.