Mkoa wa Kagera hasa wilayani Muleba, wakulima na wakazi wake ambao hutegea zao la ndizi kama chakula kikuu eneo hilo, hivi sasa wanakabiliwa na njaa kali kutokana na migomba kushambuliwa na mdudu maarufu kwa jina la mnyauko. Ugonjwa huu ni hatari sana na umekausha kabisa mashamba mengi eneo hilo.
Wakazi hao kwa sasa wanategea chakula cha kununua kutoka nje ya eneo lao jambo ambalo ni gumu pia kwani familia nyingi hazina fedha baada ya zao la biashara wanalolitegemea kufanya vibaya kwa kukosa mvua za kutosha hivyo kahawa kuharibika. (Picha zote na Edson Kamukara)